JOYCE KIRIA AFUNGUKA YAKE YA MOYONI, KAMA UNATAKA KUJUA SOMA HAPA KAELZA KILA KITU
"MAELEZO YANGU HAYA YATAONDOA UTATA WOTE NA HOPE MTANIELEWA" Kiruuuuuuuuuuuuuuuu wananchi wenye hasira kali angalieni msinitoe roho!
Kwa yeyote niliyemkwaza anisamehe bureeee..
Wacha niwape uzoefu-
1. Ndoa ya kwanza nilichangisha kama UTAMADUNI wa wengi kwenye jamii yetu... Lakini
Pamoja na michango tena mingi, tuliingia gharama zetu kubwa sana, na
kama haitoshi tulikopa. Baada ya shughuli tulianza KUPIGA MIAYO YA NJAA
hatuna ela na madeni juu..binafsi nilijuta sana lakini siku zote MAJUTO
ni Mjukuu...(siku isiyokuwa na jina Ndoaikasambaratikia****)
2.
Ndoa ya pili.(BOMANI/SERIKALINI)Mungu akanikutanisha na Henry Kilewo
anaejua nini maana ya Mke, anaeniheshimu na kunitunza, anaenipenda na
kunijali. Henry akaandaa sherehe NDOGO SANA ndugu jamaa na marafiki
WACHACHE sana, kwa GHARAMA ZAKE. Mume wangu Henry Hakusumbua mtu yeyote.
Baada ya lile tukio wala hatukupata ile adha ya madeni na kuishiwa pesa
kabisa ndani. Tukaendelea na maisha matamu kwa Upendo na Uaminifu mpaka
sasa.
3.KUMUHUSISHA MUNGU KWENYE TENDO/ KUBARIKI NDOA.. Kwa
Mkristo hili ni tukio kubwa sanaaaaaa. Mungu wetu husamehe makosa
yoooote tunayotenda hapa duniani haijalishi! Ukirudi kundini unasamehewa
kila kitu. Ndivyo tulivyofanya jana tulirudishwa kundini kisha
TUKABARIKIWA. OOOH MY LORD JESUS THANK U SO MUCH KWA REHEMA NA NEEMA.
HAKUNA WA KUFANANA NA WEWE YEHOVA. kama Mungu amenisamehe wewe ni nani
hata unihukumu??. lets go back to the story
Ningekuwa
na mawazo mgando ningefanya sherehe ya kukata na shoka.. kwanza kutetea
jina langu(umaarufu mavi) na kuwazodoa waliochonga sana kwamba kanisa
nitalisikia kwenye tv na redio na magazeti)
Mazoea- kwa hiyo watu
wengi huwa wanafanya sherehe kubwa sana haijalishi anaanza au
anaendelea ili KUWAFURAHISHA WATU WENGINE.....na hasa akiwa na jina
mjini Atajitutumua hata kama uwezo hana atafanya kila awezalo aweke
heshima uchwara mjini.
Mimi
Joyce Kiria namshukuru Mungu amenipa Akili za Maisha siyo za darasani
za kukopi na kupesti. Nilizotumia wakati ule ikala kwangu! Ningekuwa
na Akili za kukopi na kupesti NINGEFANYA PATI KUBWA SANA BILA
KUCHANGISHA MTU kwa sasa namshukuru Mungu si haba uwezo wa sherehe
ninao, NA HATA NINGEAMUA KUCHANGISHA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NINGEPATA
PESA NYINGI SANA KWA TAARIFA YAKO.
HITIMISHO. TZ ndo nchi iliyobaki tunachangisha sherehe. Jirani zetu wanachangia ugonjwa na Elimu. Tukubali kubadili mitazamo yetu.
Kama unauwezo wa kufanya Sherehe fanya kwa sababu ni jambo jema sana. Usiwasumbue watu kwa michango. Haina maana hata kidogo. Kwa
sisi ambao hata uhakika wa maisha bora hatuna, tunaishi tu bora
kumekucha tunamshukuru Mungu, siyo lazima tuchangishe watu, tujikite ktk
kuboresha maisha yetu ili baadae tufanye sherehe bila kutegemea
michango, michango ni shida kubwa sana. Kama kuna watu waliomaliza
salama bila kubaki na umasikini ni wachache sana...
Au tuendelee
kuchanga lakini hizo fedha zikatusaidie kwenye maisha. Wahusika
wakaanzishie miradi ya kuwasaidia. Siyo kula kunywa na kucheza kwaito
hapana aiseeeee...
Pia jana tulibatiza Watoto wetu ambao Tunawapenda sana. Tungeweza pia kufanya sherehe kubwa...
Kwa
kuwa hatukufanya Sherehe na uwezo tunao, mwakani tutawapeleka Shule
watoto kadhaa wenye uhitaji kwenye jamii yetu. Yule binti aliyeshindwa
kufanya mtihani wa 4m4 kule rombo, tutampeleka private kwa sababu
walisema hawana uwezo huo ndo maana alikuwa tayari kuendelea kusoma
wakati mtoto akiwa na wiki kadhaa toka azaliwe, wale watoto 3 wa Stela
aliyekatwa mkono huko dodoma kama unawakumbuka, watoto 2 wa Gati Chacha
aliyekatwa mguu huko Tarime Mara n.k
Tuchangie maendeleo tuachane na sherehe....Kenya wameweza kwa nini TZ tushindwe?!
Wanangu
nitawasihi sana wasifanye SHEREHE bali wasaidie wengine au waanzishe
miradi na kama wana uwezo basi wafanye bila kuathiri uchumi wao na
wasisumbue watu.
No comments:
Post a Comment