Tuesday, 23 April 2013

Je ni sawa kwa watoto kutumia tabiti ?


Watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, wana kiu kikubwa kutaka kujua mambo ya teknoplojia mpya.

Kutoka kwa Smart phone hadi kwa tabiti na michezo ya komputa sio nadra kuwaona watoto wakishika skrini za vifaa hivyo na kubonyeza kwenye simu.

Hata kama wazazi wanafurahia kimya kinachojiri wakati anapompa mtoto wake kifaa chochote cha teknolojia kuchezea, wazazi huwa na wasiwasi kuwa skirini hizi zinaathiri akili za watoto.


Lakini inaonekana kama skrini zinaweza kuwa na manufaa kwa watoto hasa kwa kusoma na hata kuweza kujua mambo tofauti.
Utafiti wa chuo kikuu cha Wisconsin uliowasilishwa katika mkutano kuhusu ukuwaji wa watoto, ulionyesha kuwa watoto walio na umri kati ya miaka miwili na mitatu, wana uwezo wa kugusa skirini ambazo ni za kuteleza na kuelekeza kuliko zile ambazo hazina hilo.
Watoto wenye kutumia simu za Smartphones na Tabiti, wanakuwa bora zaidi ikilinganishwa na wenzao kwani wanafanya makosa machache na kujifunza haraka pia ikilinganishwa na wenzao.
Hii bila shaka ni afueni kwa wazazi , watoto wenu wanafanya kile kinachokuja chenyewe na kutangamana na dunia.
Hata hivyo teknolojia kwa mfumo wa simu na tabiti , itasalia kukuwa. Shule nyingi za msingi na shule za chekechea zimeanza kutumia tabiti katika madarasa ili kuendeleza masomo.
Teknolojia na kuelewa ambavyo vifaa vinafanya kazi pamoja na teknolojia ya mawasiliano ni sehemu ya mitaala ya shule.
"mimi sio mmoja wa watu walio na dhana kuwa hatupaswi kuwaruhusu watoto wetu kutumia simu za mkononi na tabiti,''anasema Helen Moylett, wa shirika linalolenga kuinua viwango vya elimu miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

"vinaweza kuwa vifaa vizuri sana kwa masomo ya watoto kuwasaidia lakini sio wakati wote.''
Lakini wasiwasi wake mkubwa ni kuwa wazazi huwa sio mfano mzuri ambao watoto wanaweza kuwaiga.
''Huwa naona wazazi wakituma ujumbe wa simu ya mkononi wakitembea. Wakati mwingi, wanatumia sana kupita kiasi hadi kutokuwa na muda na watoto wao.''
Mwanasaikolojia mmoja Daktari Aric Sigman, amekuwa akisema kuwa watoto huja kuzoea vifaa hivyo sana hali ambayo inaweza kusababisha shinikizo la mawazo kwa watoto wanapopokonywa.
Anasema kuwa watoto watakuwa wametumia mwaka mmoja wakitumia simu au tabiti wakati wanapofika umri wa miaka saba.
Ikiwa ni kweli watu wachache wanaweza kupinga kuwa hoja hii inaogofya.
Inaarifiwa kuwa watoto walio chini ya umri wa miaka sita kwenda chini, wanapaswa kutumia saa mbili kwenye vifaa hivyo na hiyo inatosha kwa siku nzima.
Ingawa kuna wachache wanaoonelea kuwa skrini sio nzuri kwa afya ya watoto, hakuna ushahidi kuonyesha kuwa zina athari kubwa.

No comments:

Post a Comment