Monday, 22 April 2013

Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea.

NewsImages/6868502.jpg
Suarez akizamisha meno yake kwenye mkono wa Ivanovic.

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez ambaye haiishi vituko ameingia kwenye sakata jingine kwa kuzamisha meno yake kwenye mkono wa beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic. Wakati mambo yakiwa si shwari kwake, Mike Tyson amejiunga kwenye twiter ya mshambuliaji huyo wa Liverpool.

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez ambaye aliwahi kufungiwa mechi saba kwa kumng'ata mchezaji mwenzake shingoni Otman Bakkal, wakati akicheza kwenye ligi ya Uholanzi, ameingia kwenye sakata jingine kwa kumng'ata beki wa Chelsea,Branislav Ivanovic.

Suarez ameomba radhi kutokana na kitendo chake cha kumng'ata mkononi Ivanovic wakati timu hizo mbili zilipocheza jumapili jioni kwenye mchezo wa ligi kuu soka nchini Uingereza.

Suarez,amesema binafsi anasikitishwa na kitendo alichokifanya na amempigia simu Ivanovic na kumuomba radhi yeye mwenyewe kwani anajutia kitendo alichomfanyia.

Kitendo hicho kilitokea katika kipindi cha pili cha mechi baina ya Liverpool na Chelsea.Mechi iliyoishia kwa sare ya 2-2 huku Suarez akifunga bao la dakika za mwisho la kuisawazishia Liverpool.

Ivanovic alimuonyesha mwamuzi Kevin Friend sehemu aliyong'atwa na Suarez lakini mwamuzi alionekana kutotilia maanani kwa kuwa hakukiona kitendo hicho.

Bingwa wa zamani wa ndondi za uzito wa juu duniani, Mike Tyson ambaye alinyofoa kipande cha sikio la Evander Holyfield mwaka 1997, amechochea moto sakata hili kwa kujiunga kuifuatilia twiter ya Suarez.


No comments:

Post a Comment