Hatimaye jina la Oneza limefikia tamati jana baada ya Afrika kuamua kumuondoa shemeji yetu Oneal aliyepata kura ndogo zaidi katika The Chase.
Pamoja na matumaini madogo sana aliyokuwanayo Feza ya kupona panga la eviction ya jana (August 4) lakini Afrika imeamua kummbakiza Feza mshiriki pekee wa Afrika mashariki na Tanzania aliyebaki.
Feza Kessy amepona katika eviction ya jana kwa kura tatu tu za Tanzania, Kenya na Sierra Leone , wakati Uganda wakiwa kama nchi ya Afrika mashariki wameonekana kuchoshwa na mapenzi ya Oneza hivyo kura yao wakampa Bimp.
Bimp ndiye mshiriki aliyekuwa star wa eviction show ya jana sababu ndiye aliyepata kura nyingi (6) na alikuwa akizungumziwa zaidi na watazamaji wa nchi mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.
Katika Eviction show ya jana washiriki watatu waliokuwa kikaangoni ni
Nigeria ndio nchi pekee ambayo bado inawakilishwa na washiriki wawili mpaka sasa ambao ni Beverly na Melvin. Nchi zilizosalia na muwakilisho mmoja mmoja ni Tanzania (Feza), Afrika Kusini (Angelo), Ethiopia (Bimp), Zambia (Cleo), Namibia (Dillish), na Ghana (Elikem)
Sasa ndio naweza kusema ‘now the chase is on’, leo ikiwa ni siku ya 71 ya mchezo na kumbuka zimebaki siku 20 tu kukamilisha siku 91 za msimu wa 8 wa Big Brother ambayo sasa imebaki na washiriki 8 tu ambao watano kati yao ndio watakaoingia fainali. Tuwe wazalendo kwa kuendelea kumpigia kura Feza endapo ataingia hatarini muda wowote.
Hivi ndivyo Afrika ilipiga kura
Angola: Bimp
Botswana: Oneal
Ghana: Bimp
Kenya: Feza
Ethiopia: Bimp
Malawi: Bimp
Namibia: Bimp
Nigeria: Bimp
South Africa: Oneal
Sierra Leone: Feza
Tanzania: Feza
Uganda: Bimp
Zambia: Bimp
Zimbabwe: Bimp
Rest of Africa: Bimp
Total: Bimp = 10, Feza = 3, Oneal = 2
No comments:
Post a Comment