Polisi nchini Zanzibar wameahidi kutoa zawadi ya
shilingi milioni 10 za Tanzania kwa yeyote atakayetoa taarifa
zitakazopelekea kukamatwa kwa watu waliowashambulia wasichana wawili
waingereza kwa Tindikali.
Wasichana hao kutoka London, Kirstie Trup na
Katie Gee, walirushiwa Tindikali kwenye nyuso zao walipokuwa wanatembea
mjini Jumatano Jioni.
Kristie Trup na Katie Gee
Serikali ya Zianzibar ndio itakayotoa zawadi hiyo.
Polisi wanasema kuwa hizo ni pesa nyingi sana kisiwani Zanzibar.
Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa
miaka 18 kutoka London, walipelekwa hospitalini nchini Tanzania baada ya
kushambuliwa Mashariki mwa kisiwa hicho.
Inaaminika kuwa walitoka Tanzania kuelekea Uingereza Alhamisi usiku.
Mama za wasichana hao, Rochelle Trup na Nicky
Gee, walielezea kughadhabishwa mno na shambulizi hilo ambalo sababu yake
haiwezi kujulikana na ambalo halikuchochewa kivyovyote. Walishambuliwa
na wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki.
Polisi walisema kuwa walirushiwa Acid kwenye nyuso zao, kifuani na kwenye mikono yao walipokuwa wanatembea mjini .
Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliowashambulia walitoroka na polisi hawajui kwa nini wanawake hao walilengwa.
Mama za wasichana hao walisema kwenye taarifa
yao kuwa walighadhabishwa mno na shambulizi hilo na hawaelewi kwa nini
wasichana hao walishambuliwa ili hali walikwenda Zanzibar kwa nia njemaTunashukuru kwa wale wanaotaka kujua kinachoendelea lakini tungeomba
vyombo vya habari vituwache kwa sasa hadi tutakapokutana na watoto
wetu,'' alisema msemaji wa familia za wasichana hao.
Wasichana hao walikuwa wamekaa Zanzibar kwa muda
wa wiki mbili ingawa walitarajiwa kuwa huko kwa wiki tatu, kupitia kwa
kampuni ya usafiri ya i-to-i Travel, ambayo ilisema inafanya kila
iwezalo kuwarejesha nyumbani Uingereza.
Kari Korhonen, mkurugenzi mwenza wa kampuni
ambayo wasichana hao walikuwa wanafanyia kazi, alisema kuwa hali yao si
mbaya ikizingatiwa athari za Acid kwa mwili na visa ambavyo vimewahi
kushuhudiwa vya kuchomwa kwa Tindikali
Msemaji mwingine aliongeza kuwa wasichana hao walikuwa njiani kuelekea kwa maankuli ya jioni wakati wa shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment