Tuesday, 13 August 2013
RUVUMA: MKE APEWA TALAKA KWA KUMJERUHI MUMEWE
Na Steven Augustino, Tunduru Mkazi wa Kijiji cha Mchuluka Wilayani Tunduru Abdalah Njuga (23)
amelazimika kutoa talaka kwa Mkewe baada ya kumtuhumu kumjeluhi kwa kumvuta sehemu zake za Siri na kumsababishia maumivu makali.Kufutia hali hiyo Njuga amelazimika kumtaliki mkewe huyo na kuachana nae kwa madai kwamba maamuzi hayo yametokano na hofu ya kuendele kupata madhala zaidi endapo atashidwa kuihuduma familia yake hiyo kutokana na ufukala wa kipato alionao.Akiongea kwa Shida Njuga ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru Njuga alisema kuwa chanzo cha Tukio hilo ni mkewe huyo
kumtuhumu kushindwa kuwahudumia yeye pamoja na watoto wake katika kuwanunulia vifaa vya sikukuu ya Eidd.
Akifafanua taarifa hiyo Njuga alisema kuwa katika tukio hilo mkewe huyo ambaye alimtaja kwa jina la Sauda njuga au Mama Maria alisema
kuwa katika tukio hilo pamoja na kumvuta nyeti hizo pia alimpiga kwa kutumia mti na kumuuma meno sehemu mbali mbali za mwili wake.
Alisema ugomvi ambao ulianza usiku wa manane Mkewe huyo ghafla alicharuka na kuanza kumshambulia na baadae kumvuta sehemu zake za
siri ambapo baada ya tukio alikimbizwa katika Zahanati ya Kijiji hicho kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza.
Manga mfawidhi wa hospitali hiyo dkt.Joseph Ng’ombo alisema kuwa hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.
Alisema katika tukio hilo majeruhi huyo aliumizwa vibaya sehemu zake za siri pamoja na kupata majeraha makubwa mwilini mwake kutoka nakipigo hicho.
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment