Ngassa
In Summary
Iwapo suala la Ngassa litashindikana kuamriwa
kisheria, ina maana kuwa wajumbe wa kamati hiyo watapiga kura na hiyo
itaifanya Yanga kuibuka kidedea kwani ina wajumbe wanne dhidi ya watatu
wa Simba.
KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) inakutana kwa siku mbili kuanzia kesho Jumatano kujadili
utata na pingamizi za usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu Bara, lakini
Yanga inaonekana kuwa na faida zaidi kuliko Simba kuhusu suala la Mrisho
Ngassa.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF
inaundwa na wajumbe saba na hao ndio watakaoamua uhalali wa Ngassa
pamoja na wachezaji wengine waliowekewa pingamizi.
Wajumbe saba wanaounda kamati hiyo ni pamoja na
Mwenyekiti; Alex Mgongolwa, Makamu Mwenyekiti; Hussein Mwamba pamoja na
wajumbe; Llyod Nchunga, Imani Madega, Ismail Aden Rage, Omari Gumbo na
Venance Mwamoto.
Hata hivyo, katika kamati hiyo, wajumbe wanne ni
wapenzi wa Yanga na wajumbe watatu ni wapenzi wa Simba, hivyo iwapo
suala la Ngassa likifikia hatua ya kupiga kura ni dhahiri kuwa Yanga
itashinda kutokana na kuwa na wajumbe wengi katika kamati hiyo.
Wajumbe ambao ni wapenzi wa Yanga ni Mgongolwa, Madega, Nchunga na Mwamoto.
Simba itakuwa na wajumbe watatu tu; Rage, Gumbo na Mwamba.
Iwapo suala la Ngassa litashindikana kuamriwa
kisheria, ina maana kuwa wajumbe wa kamati hiyo watapiga kura na hiyo
itaifanya Yanga kuibuka kidedea kwani ina wajumbe wanne dhidi ya watatu
wa Simba.
Lakini faida nyingine ya Yanga katika kikao hicho
ni kwamba itakuwa na wanasheria watatu wakati Simba haina mwanasheria
hata moja.
Wanasheria hao ni Mgongolwa, Madega na Nchunga ambao wanaweza kutumia vifungu kadhaa kuimaliza kesi hiyo ya Ngassa kirahisi.
Hata hivyo, kamati za TFF hutumia kanuni na sheria
za soka katika kuamua mambo hayo, hivyo suala la upenzi wa timu
linaweza lisiwe na nguvu yoyote.
Kamati hiyo msimu uliopita iliwaidhinisha Mbuyu
Twite na Kelvin Yondani kuchezea Yanga baada ya kubaini kuwa mikataba
waliyosaini Simba ilikuwa na utata.
Ngassa alisaini mkataba wa mwaka moja akiwa kwa mkopo Simba akitokea Azam, kabla ya Yanga kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
No comments:
Post a Comment