Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas. |
Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi baada ya kufanya jaribio la kuiba simu na fedha katika duka moja maeneo ya Shamsi jijini hapa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas amesema hivi karibuni kuwa mwanamke huyo alikamatwa baada ya kuingia katika duka moja akiwa na mwanaume mmoja jambazi na kumtishia muuzaji ili awape fedha za M-Pesa na simu zilizokuwepo dukani humo huku akiwa na bastola mkononi.
“Kulikuwa na mteja mmoja jirani ambaye alimpiga kichwa mwanamke huyo na akaanguka chini, purukushani ikaanza na yule mwanaume aliyekuwa naye akakimbia na kwa kuwa kulikuwa na askari doria walikuwa wanapita eneo hilo, walimkamata mwanamke huyo,” alisema
kamanda Sabas. Akifafanua zaidi, kamanda huyo alisema alipofikishwa kituo kikuu cha polisi alihojiwa na kuwataja wenzake wanne ambao baada ya msako walikamatwa na walipopekuliwa nyumbani kwao walikutwa na shotgun moja, risasi, simu ya upepo pamoja na sare ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na buti zake.
No comments:
Post a Comment