KWA
kawaida mwanaume ana korodani mbili ambazo zimehifadhiwa katika mfuko
maalum wenye tabaka tatu na ndani kuna kiasi kidogo cha maji
kinachozunguka korodaniili kuilinda. Mwanaume endapo atakuwa na korodani
moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo kubwa. Kazi
ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume, mwanaume anaweza kuwa na
korodani zote mbili lakini akashindwa kuzalisha mbegu za uzazi kutokana
na matatizo mbalimbali tuliyoelezea katika toleo lililopita.
Mwanaume mwenye korodani moja anaweza kuzalisha mbegu au asizalishe kabisa, kitu cha msingi akapimwe hospitali kuona
uwezo wa hiyo moja. Mwanaume ambaye hana korodani kabisa hawezi kuzalisha mbegu za uzazi hivyo hana uwezo
wa kumpa mimba mwanamke. Tatizo la kuwa na korodani moja au kukosa kabisa tutakuja kuliona katika makala zijazo.
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Maumivu
ya korodani hutokea katika korodani au haswa moja au zote mbili endapo
zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi. Maambukizi haya yanaweza kuwa
makali na ya muda mfupi,yanakuwa makali kwa muda fulani halafu yanapoa
yenyewe au kwa dawa baadaye yanarudi tena yakiwa makali sana kama mwanzo
au pia huwa sugu yaani unakuwa na maumivu ambayo siyo makali ila ni ya
muda mrefu na yanayokunyima raha. Maumivu ya korodani yanaweza kuwa
makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani
inavimba kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo
hili kitaalam huitwa ‘Fournier’s gangrene’ au inatamkwa ‘Fonias
gangrini’.
Vilevile
inaweza kutokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha ukapata
maumivu makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni, tatizo hili linaitwa
‘Testicular Torsion’. Matatizo haya kwa ujumla wake tutakuja kuyaona
katika makala zijazo.
CHANZO CHA TATIZO
Maumivu
ya korodani yana vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale
yanayochukua takriban zaidi ya miezi mitatu. Maumivu makali na ya ghafla
huwa
hayavumiliki na huwa na tiba ya dharura. Maumivu haya sugu huwa kwa
kipindi fulani hasa kwa wanaume ambao wametoka kufunga uzazi ‘Vesectomy’
lakini baadaye hupoa. Vilevile husababishwa na maambukizi katika
korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits, Prostatis na Orchitis
ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi vya mwanaume na husababisha
ugumba.
Tutakuja
kuona katika matoleo yajayo. Vilevile korodani inaweza kuwa na vivimbe
kwa ndani,pembeni au juu ya kokwa au kuizunguka. Uvimbe au vivimbe hivi
vinaweza kuwa na mishipa ya damu iliyojikunja humo, kujaa maji isivyo
kawaida, mbegu za kiume kujikusanya na kushindwa kutoka na mengine ya
kitaalam ambayo pia tutakuja kuyaona.
Yote
haya humsababishia mwanaume ugumba. Maumivu pia husababishwa na kuumia
korodani au baada ya kufanyiwa upasuaji kama tulivyokwishaona hapo
awali. Maumivu yatokanayo na korodani au kende kujinyonga huwa makali
sana na korodani zikiguswa
huuma sana na kawaida huendelea hivyo kwa masaa yasiyozidi sita.
No comments:
Post a Comment