...Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.…
Toyota Noah yenye namba za usajili T502 AUP iliyokuwa ikitoka wilaya ya Gairo kuelekea Morogoro mjini baada ya kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB.
Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora baada ya kugongana uso kwa uso na Toyota Noah yenye namba za usajili T502 AUP.
Watu saba wamepoteza maisha katika ajali huyo akiwemo dereva wa Noah aliyejulikana kwa jina la Masoud Juma na wengine wanne hali zao ni mbaya.
"Chanzo cha ajali hii ni dereva wa Noah ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla akakutana na lori uso kwa uso" Alisema Bw. Sanjo Ole ambaye ni mfugaji jamii ya Kimasai.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment