Friday, 22 November 2013

KWA MARA YA KWANZA, MESS AMSIFIA RONALD KWA JINSI AFUNGAVYO MAGOLI..!!

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ameusifia uwezo wa ufungaji magoli wa mpinzani wake, Cristiano Ronaldo wakati ambapo kuna uwezekano mkubwa mchezaji huyo wa Ureno anaweza kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa Fifa mwaka huu.
Akiongea na mtandao wa Marca, Messi alisema: “Sijui kama Cristiano Ronaldo yupo kwenye kilele chake lakini siku zote huwa yupo pale kufunga kwenye michezo yote na kuchukua sehemu kwenye klabu na timu yake ya taifa. Amekuwa akifanya hivyo kwa miaka mingi na hata kama akiwa kwenye kilele ama chini kidogo hakuna tofauti.”
Ronaldo, 28, anaonekana kuwa nafasi ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka dhidi ya Messi.

No comments:

Post a Comment