KLABU ya Manchester United lazima iamue kumpeleka Danny Welbeck kufanyiwa upasuaji wa goti ambao utamuweka nje mshambuliaji huyo wa England kwa wiki nyingine tano.
United tayari inamkosa kiungo Michael Carrick, ambaye atakuwa nje hadi Krisimasi kwa majeruhi.
Majeruhi: Danny Welbeck atalazimika kufanyiwa upasuaji wa goti ambao utamuweka nje kwa wiki nyingine tano
Pigo United: Michael Carrick atakuwa nje hadi Krisimasi kwa majeruhi
Matatizo yanayomsumbua Welbeck tayari yamemfanya amekosa mechi sita zilizopita za United.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anapatiwa matibabu yanayompa matumaini anaweza kuepuika upasuaji, lakini United inahofia italazimika kumpeleka kwenye upasuaji ikiwa hali yake haitaimarika.
Welbeck amekwishafanyiwa upasuaji wa goti mara mbili. Marouane Fellaini pia anaweza kuwa nje kwa wiki hadi 10 atakapofayiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia.
Carrick alikwenda kwenye ziara ya mashindano ya dunia ya DP Dubai
Carrick aliungana na Caroline Wozniacki kumtazama Rory McIlroy akicheza
David Moyes atawakosa Carrick na Welbeck katika mechi na Spurs na Everton
No comments:
Post a Comment