Baaada ya Staa wa sinema na muziki Bongo, Snura Anton Mushi na
Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa kunaswa kimahaba
hapo jana, leo Mwanadada Snura Mushi amfunguka na kudai kuwa Ngassa ni
rafiki yake tuu na si vinginevyo
“Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi
na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo
zangu.Ngassa alinitembelea kama marafiki wengine
wanaokuja nyumbani kwangu. Simu yangu ilipotea ndiyo maana picha
zikavuja lakini ukweli ndiyo huo.”
Kwa upande wake Ngassa ambaye yupo mapumzikoni baada ya kumalizika
kwa msimu wa kwanza wa Ligi Kuu Bara hakuweza kusema chochote kufuatia
simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.
Hapo awali ilidaiwa kuwa wawili hao walibambwa wakiwa wamejiachia ‘wakifanya yao’.
Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali
macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na
majirani zake.“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila
kificho chochote.
“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
“Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele
za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.
Ili kujiridhisha, Tulisaka picha za wawili hao ambazo walikuwa
‘wakijifotoa’ kwa simu zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo lililozua
utata na maswali kwa walioziona.
Uchunguzi ulibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa Snura na Ngassa
kunaswa wakiwa beneti kwani wiki mbili zilizopita walibambwa kwenye
ukumbi mmoja wa starehe jijini Dar
No comments:
Post a Comment