Wednesday, 27 November 2013

STEVE RnB WA 'JAMBO JAMBO'AMVISHA PETE MCHUMBA WAKE WA TOKA SECONDARY.


Hit maker wa ‘Jambo Jambo’ Steve RnB amefungua ukurasa mwingine wa mapenzi baada ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi ikiwa ni kiashirio cha kuelekea katika ndoa.

Kwa mujibu wa VIBE, Steve ambaye pia ni memba wa bendi ya In Africa amemvisha mpenzi wake huyo anayesemekana kuwa ni wa toka enzi zao za shule.

Kwa picha hii (hapo juu) inaonekana Steve hakutaka kufanya party wala kuifanya kitu kikubwa zaidi ya kuwasilisha ombi lake wakiwa kibarazani na kumwambia kipenzi chake ‘will you marry me’? Hopefully jibu lilikuwa Yes!

Hongera kwa Steve tunawatakia safari njema ya kuelekea kwenye ndoa yeye na mchumba wake.

No comments:

Post a Comment