Polisi akimpa kichapo dereva daladala.
WAKAZI wa mjini hapa wamekilaani kitendo cha askari wa kituo kikuu cha
polisi baada ya kumpa kipondo na kumkwida hadi kumvua nguo hadharani
dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Bello.Tukio hilo lililojaza umati wa watu lililoshuhudiwa na paparazi wetu
lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya stendi ya daladala mjini
hapa.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema Bello aliyekuwa akiendesha gari aina ya
Toyota Hiace inayofanya safari zake kati ya Mjini na Mazimbu,
alikamatwa kwa kudaiwa kuegesha gari vibaya.
“Stendi ni ndogo Bello aliegesha gari lake akisubiri foleni yake ili
apakie, cha ajabu askari akafika na kumpa kibano kabla ya kumsweka
ndani,” alisema Wamaga Juma na kuongeza:
Kutokana na kichapo kutoka kwa polisi, nguo za dereva daladala zilivuka.
“Wananchi wenye hasira walitaka kumzingua askari yule, akapiga simu na
kuwaita wenzake wa kikosi cha usalama barabarani, walipofika walimbeba
Bello na kumpeleka kituoni huku akiwa na kipensi tu.”
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliwapongeza askari hao kwa madai kuwa,
madereva wengi wamekuwa wakivunja sheria za barabarani hivyo kibano
alichopewa Bello kitakuwa fundisho kwa wengine.
No comments:
Post a Comment