Thursday, 19 December 2013

Kikongwe wa miaka 87 amuua kijana kwa Risasi kisa kikiwa ni Ugomvi wa Ardhi huko Kahama....Wananchi wakasirika na kumuua Kikongwe huyo kinyama...!!

Migogoro ya kugombea ardhi imeendelea kusababisha vifo baada kikongwe mwenye umri wa miaka 87 mkazi wa kijiji cha Kahanga wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga kumuua kwa kumpiga risasi ya kichwa mkazi mmoja wa kijiji hicho kutokana na ugomvi wa mashamba.




Hata hivyo kikongwe huyo aliyetajwa kwa jina la Charles Makune (87) naye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira waliofika katika eneo la tukio kwa lengo la kutaka kuamua ugomvi wa watu hao wawili. 

Mauaji hayo yametokea ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina, kuuawa na wananchi wenye hasira kutokana na ugomvi wa kugombea ardhi. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala, amemtaja aliyeuawa kwa kupigwa risasi na kikongwe huyo kuwa ni Mihangwa Maziku (40) maarufu kwa jina la Mambe, mkazi wa Kijiji cha Kahanga na kwamba tukio hilo lilitokea Desemba 15, mwaka huu saa moja asubuhi kijijini hapo. 
 
 

No comments:

Post a Comment