Huenda Rais Uhuru Kenyatta akalitangaza Baraza la Baraza la mawaziri wiki hii.
Nairobi.Baraza la mawaziri nchini Kenya linangojewa kwa hamu na wananchi ambapo wangi wanatarajia liwe la mseto kama ilivyo Katiba ya Kenya.
Nairobi.Baraza la mawaziri nchini Kenya linangojewa kwa hamu na wananchi ambapo wangi wanatarajia liwe la mseto kama ilivyo Katiba ya Kenya.
Taarifa kutoka Kenya ambazo ni za kuaminika zimesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kutangazwa kwa Baraza hilo kati kati ya wiki hii.
Pia Taarifa zilifichua kwamba washirika kwenye muungano wa Jubilee bado wanajadiliana kuhusu ni upande upi utatoa nafasi kwa baadhi ya vyama vidogo vilivyotia sahihi mkataba wa maelewano baada ya uchaguzi mkuu kwa lengo la kuimarisha utawala wa Jubielee.
Kutokana na hali hiyo raia wa Kenya wamekuwa wakisubiri kwa hamu kusikia baraza jipya la mawaziri likitangazwa .
Taarifa ziliendeela kudodosa kwamba mahojiano na washirika wa karibu wa viongozi yalionyesha kuwa viongozi hao wameamua kubadilisha kabisa muundo wa utawala.
Kwa sasa anachokifanya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na timu yake ,anaandaa majina ya baraza lake la Mawaziri na pia makatibu,wakuu wa mashirika pamoja na nyadhifa zingine za juu wakiwemo wakurugenzi wa Wizara na Idara.
Hiyo ina maana kuwa Wakenya watajionea baraza jipya kabisa la mawaziri, makatibu wapya, mabalozi, maofisa wakuu wa mashirika ya serikali na wakurugenzi wa wizara na idara mbalimbali.
Hata hivyo awali Rais Kenyatta alishatoa ahadi ya kulitangaza baraza lake la mawaziri wapya huku akizingatia taaluma, utendaji wa kazi, uwakilishi wa kimaeneo na jinsia.
Kutokana na hali hii, baadhi ya mabalozi walioagizwa warejee nyumbani huenda wasirudi katika nafasi zao za awali.
Kutokana na hali hii, baadhi ya mabalozi walioagizwa warejee nyumbani huenda wasirudi katika nafasi zao za awali.
No comments:
Post a Comment