Monday, 22 April 2013

Wabunge wa Uganda wakamatwa India




Kampala. Polisi wa India wanawahoji wabunge wa Uganda kwa kujaribu kujipatia kiasi cha fedha 50 bilioni za udanganyifu kutoka kwa wakurugenzi wanne wa Videocon na makao makuu ya kampuni ya kuzalisha umeme nchini humo.
Vigogo hao wa  Serikali waliokumbwa na kashfa hiyo ni pamoja na Mbunge wa zamani wa Buzaya ,ambaye pia alikuwa waziri wa Mambo ya Mikoa Issac Musumba.
Wengine ni mbunge wa  Igara  Kata ya Mashariki Michael Mawanda, na mfanyabiashara mkubwa nchini Uganda Yakuba Mathai.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Katibu mkuu  wa Mambo ya Nje James Mugume alisema kwamba viongozi hao walikamatwa  katika mji wa Mumbai nchini India wakituhumiwa kujipatia kiasi hicho cha pesa.
Alisema kiasi hicho  ambacho ni , $ 20,000,000 (Shs50 bilioni)  ni kutoka katika kampuni ya Videocon na makao makuu ya kampuni ya kuzalisha Umeme nchini humo.
Alisema hiyo ni kazi ya kipolisi hivyo wanawaachia wafanye kazi yao na pia wataendelea kuleta taarifa zaidi kwa wananchi nini kinachoendelea huko.
 Siwezi kutoa maelezo mengi  kwa sasa kwa sababu sisi pia hatuna  ukweli wowote tulioupata kuhusu tukio hilo “alisema  
Taarifa zilisema kwamba  Musumba na  Mawanda ni wamiliki wa hati za kusafiria za kidiplomasia lakini kwa mujibu wa polisi wa Mumbai wakati wakihojiwa ilibainika kwamba walikuja kwa lengo la kutoa ushauri wa kisheria kwa  mfanya biashara Muthai.

No comments:

Post a Comment