Rais wa awamu ya nne wa Kenya Uhuru Kenyatta, akitangaza majina ya makatibu wakuu wa wizara nne.
WAKATI Bunge la Kenya pamoja na Baraza la Seneti ya nchi hiyo wakizidi kumwandama Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto, kuhusu hatua yao ya kushindwa kutangaza baraza la mawaziri, Rais huyo ameteuwa Makatibu wakuu wanne wa wizara nne leo.
Kitendo cha Rais Kenyatta kushindwa kutangaza majina ya mawaziri wa wizara yake na badala yake akaanza na majina ya makatibu wanne ikiwa ni wiki mbili tangu alipotangaza muundo wa wizara 18 badala ya 44 kama ilivyo kuwa kwa serikali ya Mwai Kibaki imeongeza usiri mkubwa katika serikali yake.
Taarifa za Kenyatta kuteuwa makatibu hao imelifikiaHabarimpya.com hivi punde ikiwa dakika chache baada ya Kenyatta kutangaza majina hayo.
Kwa muujibu wa taarifa hiyo makatibu hao ndiyo watakao kuwa wasimamizi wakuu wa wizara hizo, makatibu hao ni pamoja na Dr Fred Matiangi Okengo atakayekuwa katika Wizara ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano.
Mwingine ni Henry K Rotich (Wizara ya Biashara), James Wainanina Macharia (Wizara ya Afya) na Balozi Amina Abdalla (Wizara ya mambo ya nje).
Kenyatta na naibu wake Ruto wameteuwa majina hayo manne ya makatibu wakuu huku wengine 14 wakitajariwa hivi karibuni.
Kenyatta na naibu wake Ruto wameteuwa majina hayo manne ya makatibu wakuu huku wengine 14 wakitajariwa hivi karibuni.
Watu mbalimbali nchini Kenya wamekuwa wakitoa maoni mbalimbali kuhusiana na usiri uliotawala katika Ikulu ya nchi hiyo, huku kila mtu akiwa na hamu ya kujua muundo wa serikali hiyo.
Uhuru aliingia madaraka kwa tiketi ya Chama cha Jubilee akiwa na makamu wake William Ruto, ambapo walimbwaga mpinzani wao Mkuu Raila Odinga na makamu wake Kalonzo Musyoka kwa tiketi ya muungano wa CORD.
Baada ya Kampeni ya miezi mitatu, Machi 4 mwaka huu Uhuru akaibuka kidedea katika uchaguzi mkuu, ambao baadeye ulipingwa katika Mahakamu ya Juu ya nchi hiyo na wapinzani wake hao hata hivyo akashinda tena na kuapishwa April 9 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment