Zito Kabwe akifafanua jambo
WAKATI wimbi la ujambazi, na ugaidi dhidi ya watu maarufu ukiongezeka kila kukicha, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Chadema Tizo Kabwe amewataka watanzania kuacha tabia ya kuingilia masuala ya Jeshi la Polisi.
Zitto alitoa kauli hiyo, kufuatia baadhi ya watu wanaoendelea kuhoji kuhusu tukio la Mama yake mzazi Bi Shida kuvamiwa na kutishia Bastola na watu ambao hawakujulikana mara moja kuwa walikuwa na lengo gani.
Akizungumzia suala hilo Zitto alisema kwamba, "Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu."alisema Zitto.
Mbunge huyo alifafanua kwamba "suala hilo tayari liko polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule".
Aliongeza kwamba matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima na kutokana na hilo suala lake litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania, Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa.
Hata hivyo Zitto alitumia nafasi hiyo kuwa watanzania ushauri na kusema kwamba, "Ushauri- tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents” nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
No comments:
Post a Comment