Kwa kawaida sote tunapenda familia zetu kuliko kitu kingine katk maisha yetu na baadhi hupenda nakujali pia marafiki zao kama watu wao wakaribu. Ukiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu wa aina hii unatakiwa kuwa mwanaglifu sana vinginevyo utapoteza mwenza na penzi kufa kabisa.
Kwanza unachotakiwa kukumbuka ni kuwa wewe ni mtu amabe amekupenda ukubwani lakini familia na rafiki zake aliwapenda tangu anakua na upendo kati ya wewe na familia/rafiki unatofautiana japo kuwa unaweza kuhisi kuwa wanapendwa nakujaaliwa zaidi au pengine unaweza kudhani kuwa wewe ndio unapendwa/penda zaidi ya ndugu/rafiki zake kwa vile tu unachangia mambo mengi yaukubwani na yeye yalakini ktk hali halisi si hivyo.
Usisahau kuwa wewe ni mtu baki na utabaki kuwa mtu baki kwamba wakati wowote unaweza ukamtenda mwenzio au kuamua kuachana nae kwa sababu zozote zile lakini familia yako wakati wote itabaki kuwa familia yake hata wakimtenda vipi kwa vile wamechangia damu.
Sasa mpenzi mwenye kupenda watu wake (familia na marafiki zaidi) anashawishika kirahisi sana japokuwa itakuwa ngumu sana kwako kwani wakati mwingine unaweza kujihisi mpweke ndani ya uhusiano.
Unachotakiwa kufanya ni kujiandaa kupendwa na kuchukiwa (kumpendwa na yeye haina maana na ndugu zake watakupenda au wewe kuwapenda), kila mtu anahitilafu nakasoro zake hali inayotufanya tuwe tofauti hapa Duniani. Hivyo unachopaswa kufanya ni kujenga heshima kwa watu ambao ni muhimu wa mpenzi wako hilo moja.
Pili, epuka kujipendekeza na kuachia ule ushemeji-shemeji, wifi-wifi uvuke mipaka, wazazi wake waite mama na baba badala ya mama/baba'ko au jaribu kutumia mzee na Bi'mkubwa......wakatimwingine huwa wanamajina yao kama vile mama Haruna (jina la mumewe ambae ni future ba'mkwe)
Tatu, mpenzi anapokuja na malalamiko kuhusu watu wake hao (vijimambo vya kifamilia) ambao wewe unajua wazi kuwa anawazimia kinamna, msikilize kwa makini na wakati huohuo tafakari kabla hujatoa maoni yako kutokana na tukio. Hapa unatakiwa kuwa na uwezo wa kuelewa na kuchambua mambo haraka au angalau jaribu kuwa msikivu na muelewa mzuri.
Epuka kuungana, kumcheka, shangaa au kupingana nae ikiwa ataonyesha kutofurahishwa na mama au baba'ke au ndugu zake wengine na badala yake jaribu kumpa mawazo ya nini cha kufanya kwa mapenzi na upole.
Ikiwa haelewi kutokana na hasira zake basi tumia "tekiniki" za kumpunguzia "stress" au hasira(natumai unazijua) ili a-calm down, hiyo itawasaidia nyote wawili kuzungumza na kuelewana.
Siku ikipita na mpenzi hajazungumzia tukio la jana lilikomkasirisha usianzishe tena kwani huo utakuwa umbea sasa....wewe tulizana akianzisha kwa kukupa matokeo ikiwa alifanyia kazi ushauri wako hiyo bonus vinginevyo "uchubue" tu usizungumzie yaliyopita kwani hayakuhusu wewe bali yeye na wazazi wake, umetoa ushaui basi jua kazi yako imekwisha.
No comments:
Post a Comment