Wednesday, 24 April 2013

Mpenzi apendae kupendeza, mshawishi atangaze Ndoa!

 leo tuangalie jinsi ya kumshawishi mpenzi anaependa mitindo mzuri na ya kisasa ya uvaaji ili atangaze ndoa hii ni baada ya kufanya yote ujuayo lakini jamaa mpaka leo mwaka wa pili wa uhusiano wenu hajaonyesha dalili ya "kukupetesha" a.k.a kukuchumbia na hatimae kufunga ndoa, hasa kama wewe uko so into ndoa. Kumbuka au jaribu kwenda kupitia lilipoanzia somo hili.


Kumshawishi mpenzi anaejipenda sio kazi ngumu sana unless wewe mwenyewe sio mtu wa kupenda kupendeza au kujipenda. Unachotakiwa kufanya hapa ni kuwa "up 2 date" na mitindo ya mavazi ya kiume na hakikisha unajua mtindo wa mavazi yake kama ni:-

-Hip- hop; hapa kuna boots/raba, t-shirt, hood namara nyingi ni over-sized n.k.

-Casual; hapa anaweza kuchanganya raba/boots, jeans, kadeti, shati/polo t-shirt, suit jacket n.k.,

-Trendy; hapa usipokuwa mara nyingi kuna kuchemsha kwa vile unavaa vitu ambavyo havina muda mrefu sokoni (vipya) na huenda visisdumu kwa muda mrefu,

-Sport; raba/boots, jeans na t-shirt kwa sana n.k

Sasa wewe kama mwanamke unachopaswa kufanya hapa kamanilivyosema hapo juu ni kujua "mtindo" wa mapenzi wako na wewe ujaribu kumfanya aendelee kubaki ktk mtindo wake huo ila ongezea "chachandu" kidogo kwa kuwa unamchagulia rangi nzuri, chagua bidhaa zenye ubora na wakati huohuo ni classic (ikiwa mtindo wa uvaaji wa mpenzi wako ni "trendy" basi unatakiwa kuwa makini na mwangalifu na kujua kitu gani ni "classic" au mpito a.k.a Mdosho).



Mpenzi mwenye kupenda kupendeza siku zote atapenda kuambiwa ukweli kutokana na uvaaji wake kwamba kapendeza au hajapendeza hivyo jitahidi kuwa mkweli na muwazi ukiweza msaidie ktk upangiliaji, vilevile hakikisha unaonyesha unajivunia sana muonekano wake kutokana na uvaaji wake.


Kwame usijaribu kubadili mtindo wake wa mavai bali boresha, mfano mtu anaependa kuvaa kawaida (Casual) hata sikumoja usijaribu kumbadilisha ili avae ki hip-hop au vinginevyo ATAKUKIMBIA(hahahahaha kwani anaona humfai unataka kumbadilisha), unachotakiwa kufanya ni kuboreha "style" ya uvaaji wake.

HAYA HABARI NDIO HIYO KAZI KWAKO NA KILA LA HERI

No comments:

Post a Comment