Tuesday, 23 April 2013

Upelelezi kesi ya ugaidi dhidi ya Rwakatele wakamilika....

.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Chadema akiwa chini ya Ulinzi

WAKATI viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Meandeleo (Chadema) wakipishana kuhusu mtizamo wa kesi ya Ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wao, Wilfred Lwakatale, Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetangaza kukamilika kwa upelelezi wa kesi hiyo.
Hivi Karibu Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe aliibuka na kusema kwamba Rwakatale avuliwe madaraka yake yote ili kupisha uchunguzi huru ndani ya chama hicho, hata hivyo kauli hiyo ya Zitto ilionekana kuwa mgumu kutekelezwa kwa sababu viongozi wakuu wakitaifa wanaamini kwamba Rwatakale ameonewa na tayari wameweka nguvu kubwa na kuandaa jopo la mawakili sita wa kumtetea.
Jana Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Issaya Mulungu, alisema  upelelezi kuhusu tuhuma za vitendo vya ugaidi zinazomkabili Mkurugenzi huyo wa Chadema  na mwenzake Joseph Ludovick umekamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mulungu alisema kwa sasa jalada linaandaliwa kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya hatua zaidi. Lwakatare na mwenzake, Ludovick, wanakabiliwa na kesi ya ugaidi, katika Mahakama ya Kisutu. Watu hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kufanya mipango ya kumteka na kutaka kumdhuru kwa sumu, Dennis Msacky. Kuhusu kesi ya kumwagiwa tindikali Kada wa CCM, Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Igunga Septemba 2011, alisema tayari watuhumiwa wawili wamekwishafikishwa mahakamani.
Mulungu alisema kuhusu kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, Absalom Kibanda, tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka na matukio mengine yaliyotokea Zanzibar, upelelezi bado unaendelea na kwamba upo katika hatua mbalimbali. Aliwataka watu kuwa na subira.

No comments:

Post a Comment