Tuesday, 23 April 2013

Wanaojifungua watoto nyumbani kutozwa faini....

 
Wodi ya wagonjwa iliyopo katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga .


Mtwara. Viongozi wa Tarafa za Mahuta na Namikupa Wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara wamesema watatoza faini kati ya Sh5,000 hadi Sh10,000 kwa wajawazito watakaojifungulia nyumbani.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa wilaya hiyo wa kuhakikisha wajawazito wote wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.
Wakizungumza katika kikao maalumu kilichoitishwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa wilaya hiyo, Scholastica Sowani mwishoni mwa wiki, viongozi hao wakiwamo watendaji wa kata na vijiji, watumishi wa zahanati walisema hatua hiyo inaweza kuwa na mafanikio.
Kwa mujibu wa Sowani tarafa ya Litehu wameweza kufikia asilimia 100 ya wajawazito wote kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya, pamoja na mikakati mingine baada ya kuweka faini ya Sh10,000 kwa watakaojifungulia nyumbani.
“Kikao hili kimeshirikisha kata za Nahyanga, Lukokoda, ambapo tatizo la wajawazito kujifungulia nyumbani ni kubwa na hadi sasa wilaya tumefikia asilimia 75 ya wajawazito wanaojifungulia hospitali, kituo cha afya au zahanati” alisema mratibu huyo.

No comments:

Post a Comment