Thursday, 4 July 2013

"WIMBO MAJANGA UMENIPA DILI LA KUREKODI MOVIE AFRIKA KUSINI "– SNURA.

 MWIGIZAJI wa kike na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Snura Mushi amedai kuwa muziki ulimpa dili ya kwenda kurekodi filamu Afrika ya Kusini...


Anasema kuwa dili hilo  amelipata kutokana na  kufanya vizuri katika muziki hasa nyimbo yake ya Majanga. 


“Filamu kwa sasa inachangamoto sana .Hilo lilinifanya nirudi katika muziki huku nikichagua filamu za kuigiza na kujikita katika muziki zaidi ambao unanifanya niwe bussy sana..

" Lakini ninachofurahia kupitia nyimbo yangu ya majanga nilipoenda kuirekodia Afrika kusini Nnilipewa uhusika mkuu kuigiza filamu ya Tandeka,”anasema Snura.


Snura anadai kuwa watayarishaji walimuona na kumwita katika usahili ,  aliposhinda alipewa muswada (Script) na kuigiza kama mhusika mkuu ambaye aliigiza kwa umahiri mkubwa...

Filamu ya Tandeka imetumia lugha mbalimbali ikiwemo Kiswahili, Kizulu na Kiingereza. Snura ni msanii mwigizaji wa filamu aliyetokea katika tamthilia ya Jumba la Dhahabu.

No comments:

Post a Comment