Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu. Wanawake wengi wanalalamika kuwa hawaoni
upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume
wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.
Mara zote
hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali
huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika, muda
wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo
zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa
huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana
na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia
mbadala. Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia.
Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu.
Njia za kukusaidia
1. kucheka pamoja
Kicheko ni
mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia
pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu,
kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya
katika vyote. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu.
Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala
yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea. Kama utaanza kujizoeza hivi
ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine
kokote.
2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe
msaada na tegemeo kwa mwenzake. Jifunze kumtia moyo na kumwezesha
mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo.
Onyesha heshima katika vitu hivyo pia. Kila upatapo nafasi mpongeze
mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako mbele
yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye.
Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Zaidi
tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua na
sisi pia.
3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso
wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote. Lazima mjifunze
kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala.
Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea,
kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine
zozote za kuonyesha ukaribu kimwili. Wengi wetu huweza kufanya haya
kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au
nidhamu mbaya? au dhambi?
Kugusana ndio
mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini
umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia
kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi
waliopweke wanaotamani kuguswa.
Mguso huu wa
upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza
kuijenga lugha ya mguso wa tendo la ndoa katika mahusiano yenu.
4. Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo
vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni
kutokuwepo kwa majadiliano. Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu
hisia zao. Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata
ndoa pia hazina ukamilifu. Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia
sio mkamilifu. Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na
nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa
husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki
ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu. Mwambie umpendae yapi
yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza
katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu
utaongezeka.
5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache
maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu. Lazima tujifunze
kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika
mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile
vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu.
Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na
msameheane.
6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi
hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko. Ukaribu
na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano wetu
lazima ume halisi na sio feki. Vile tunavyoviona katika tamthilia na
filamu sio ukaribu ulio halisi. Kama tunataka tuonekane sawa na vile
tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na
mtazamo bora katika mahusiano yetu. Ukianza kupata ukaribu wa kweli
baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na
mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe
kuvitafuta vile vyote mpenzi wako alivyonavyo ambavyo hukuza ukaribu
wenu. Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.
No comments:
Post a Comment