Tatizo ambalo limekuwa likiwakuta
wapenzi wengi wanaoanzisha uhusiano wa kimapenzi wenye mwelekeo wa
maisha ya ndoa ni kuingizwa ‘mkenge’ kwa kufichwa baadhi ya tabia mbaya
na wapenzi wao.
Wapenzi
wanaoficha tabia wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuteka mapezni ya
watu, lakini baadaye wakishafanisha azma yao hujiachia na kuanza
kuwatesa wenzao.
“Sikujua kabisa kama ana tabia hizi, ningetambua mapema kama ni mhuni nisingekubali kuoana naye.”
Uchunguzi
unaonyesha kuwa wanandoa wengi mpaka sasa wanajuta kufunga ndoa na
wapenzi wao na kwamba kama wangetambua tabia za wenza wao mapema
wasingekubali kufunga ndoa.
Inawezekana
hata wewe unayesoma makala haya unajuta kiasi cha kulalamikia mwenzako
alivyobadilika tabia tofauti na mwanzo ulivyoanza kupendana naye. Hebu
fuatilia dondoo hizi ili ujue namna ya kumtabua mpenzi anayekufichia
makucha, ili usijiingize kwenye uhusiano usiokuwa sahihi.
MPE UHURU WA KUTOSHA
Watu
wengi wanapoanzisha uhusiano huwabana sana wapenzi wao kwa kuwapekulia
simu, kuwachunga watokapo na waingiapo, jambo ambalo huwafanya wahusika
kujilinda sana wakiamini wanafuatiliwa.
Ndugu
yangu usimbane mpenzi wako, mwache huru, atembee atakavyo na awasiliane
na amtakaye, wewe kaa nyuma yake ukimchunguza bila mwenyewe kujua.
“Mke/mume wangu hajali mambo haya” Hujali kumbe unamteka mwisho wa yote
utamnasa.
MPE MAJUKUMU
Ukisha
mchagua umpendaye, huwezi kutambua uwezo wake mpaka umpe majukumu ya
kufanya. Kwa mfano mtume akalipie maji, umeme au mwagize asimamie jambo
fulani.
Ukishafanya
hivyo kaa kando mwangalie, anavyoiba chenji, anavyopunguza gharama bila
kukushirikisha, lakini baadaye muulize, utashangaa alivyotibua mambo
akidhani wewe si mtu wa kujali sana, kumbe ulikuwa umemtega na hatimaye umemnasa.
MUWEKE KWENYE WAKATI MGUMU
Njia
nyingine ya kumnasa anayekufichia makucha ni kumweka katika wakati
mgumu. Wanasema rafiki wa kweli hujulikana kwa dhiki. Tengeneza dhiki
kwa makusudi na kuzitekeleza. Akikuambia naomba unitumie vocha mpenzi au
ninunulie nguo mwambie sina pesa, halafu uone kama
atakuwa na kiwango kile kile cha mapenzi. Wapo wanaume wengine wa pesa
na mishahara ya wapenzi wao, ili kuwabaini ni kuwanyima wakati mwingine.
TUMIA WATU
Katika
hali ya kawaida, majirani na marafiki wanawatambua zaidi wapenzi wetu
kuliko jinsi tunavyowatambua sisi. Inawezekana kabisa mpenzi wako akawa
mtakatifu unapokuwepo lakini ukiondoka anajiachia ile mbaya, hivyo ili
kujua tabia zake waulize rafiki na jirani zako watakusaidia kumtabua
mpenzi wako.
ANGALIA ANAVYOWATENDEA WENGINE
Wapenzi
wengi wanapokuwa wamepata wapenzi hutazama wanavyotendewa wao na
kudhani inatosha. Mtu muungwana huwatendea wengine mema. “Aa, mama naye
kanichosha kila siku anataka pesa.”
Hebu sikia kauli hii, kama
mtu analalamika kuchoshwa na mama yake itakuwaje kwako? Amka na
kutambua kuwa anakufichia makucha na ipo siku atakubadilikia hata wewe
na kukutesa. Amka usikubali kudanganywa na mpenzi mnafiki.
No comments:
Post a Comment