BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kueleza mazito kuhusu Ray, Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro ‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao.
Akizungumza na GPL, Nora alisema Ray na Johari walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni.
“Kinachowasumbua Ray na Johari ni laana yangu na kweli nimeamini Mungu analipa hapahapa duniani kwani walinifanyia mambo ya ajabu, wakanipoteza kabisa kwenye fani, walinifanya nichanganyikiwe wakijua sitapona, lakini sasa hawaelewani tena wakati walikuwa wanapendana kama pete na kidole.
“Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye akamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi mpaka waliponipoteza kwenye fani.
“Namshukuru Mungu nimejikongoja na hatimaye nimerudi tena kwenye sanaa, mabaya waliyokuwa wakinifanyia yamewarudia wenyewe, jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu kwani nakesha nikiomba na ninaamini maadui zangu wote wataumbuka mchana kweupe,” alisema Nora.
No comments:
Post a Comment