Thursday, 28 November 2013

WALIMU WAZICHAPA KAVUKAVU OFISINI WAKIGOMBEA PESA

 
Afisa Elimu msingi wilaya ya  Sengerema Bw,Juma Mwajombe alipokuwa akimvua madaraka Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Luhama kwa kosa la kutotimiza majukumu yake.
 ****************
 
AFISA Elimu wa Shule za Msingi Sengerema Mkoani Mwanza, Bw Juma Mwajombe amemvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Luhama iliyoko kata ya Katwe kwa kushidwa kutekeleza majukumu yake.
 
Amesema kuwa amefikia maamuzi hayo kutokana na mwalimu huyo kushindwa kusimamia vema majukumu yake na kutokusimamia maadili ya walimu wake wanapokuwa kazini.
 
Bw, Mwajombe amemtaja aliye mvua madaraka hayo kuwa ni Mwalimu  Maila Majula baada ya kuchochea ugomvi kati ya mwalimu Emanuel  Joely  na Mwalimu Alfonsia Ndalahwa uliosababisha walimu hao kutwangana makonde ofisini  kwa kile kinachodaiwa kuwa walituhumiana kula fedha za ujenzi wa kisima cha shule hiyo.
 
Aidha amesema kuwa Mwalimu Mkuu anapaswa kusimamia vema majukumu yake na kushauri walimu kuacha migogoro isiyo ya lazima na kuzingatia maadili ya kazi na siyo kukuza migogoro isiyo ya lazima na kusababisha walimu kutokuheshimiana sehemu za kazi.

No comments:

Post a Comment