Familia iliyohusika kumsaka kikongwe Helena Petri siku aliyopotea.Picha na Juma Mtanda |
Wakazi Kitongoji cha Gongo, Kijiji cha Mgata, Kata
ya Bwakilajuu mkoani Morogoro, ambako tukio hilo limetokea, sasa
wanaishi kwa hofu.
Baadhi yao wanalazimika kujisaidia haja ndogo na
kubwa katika makopo hasa nyakati za usiku, ndani ya nyumba zao. Tukio
hilo limebadili kabisa mfumo wa maisha na kutembea, wengi wanalazimika
kuingia ndani ya nyumba kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12:30 jioni
wakihofia kutekwa.
Tukio lenyewe
Ni saa 7 usiku, siku ya Jumatano kuamkia Alhamisi
ya Oktoba 2 mwaka huu, Eliza Steven (19) anaamka na kumnyonyesha
kichanga chake, James Peter (miezi mitatu), baada ya kilio cha mtoto
huyo mchanga kuhitaji kunyonya.
Baada ya James kunyonya na kushiba, alinyamaza
kulia, hiyo ilikuwa ni kama kumpa fursa mama yake kutoka ndani ili aende
nje kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo.
Anafungua mlango wa chumba chake na kutoka nje
kujisaidia huku akipiga jicho na kuangalia mlango wa chumba anacholala
bibi yake, anaona mlango upo wazi. Jambo hilo, hakulitilia shaka sana
kwani alikuwa na imani angeweza kukutana naye nje ama chooni, haikuwa
hivyo.
Alilazimika baadaye kuingia chumba anacholala
bibi huyo, aliangalia kitandani ili kuweza kujibu maswali yake yaliyojaa
kichwani likiwamo la kwa nini bibi yake ameshindwa kufunga mlango kama
alitoka nje? Anaanza kusema Eliza. Eliza aliendelea kueleza kuwa baada
ya kuchunguza katika chumba kile kinachotumiwa na bibi yake, Hellen
ambaye alikuwa na kawaida ya kufunga mlango pindi aiingiapo kulala,
hakumwona na kuchukua jukumu la kumwamsha mama yake mzazi, Yustina
Kasian (40) ili aweze kusaidiana naye kumtafuta.
Yustina Kasian ambaye ni mtoto wa pili kwa
kuzaliwa kwa bibi, Hellen Petri Mahunzila anasema baada ya kuelezwa
maneno yale na mtoto wake, Eliza Steven ambaye ni bibi yake alienda
katika kile chumba anacholala mama yake na kuangalia huku na huku, bila
mafanikio.
“Nilienda chooni na kuangalia ndani ya choo lakini
sikumwona, nilirudi ndani na kumwamsha mume wangu, Steven Francis (50)
ili naye atusaidie kumfuata kwani tayari hofu ilianza kutanda moyoni
mwetu na kujiuliza maswali ambayo hatukuweza kupata majibu usiku ule,”
anasema Yustina.
Mimi baada ya kuelezwa jambo hilo na mke wangu
nilitoka nje na tochi hadi chooni na kumulika ndani na kuzunguka kile
choo, sikuweza kumwona. Nilienda pia kumtafuta kwenye banda la kupikia
na eneo zima la migomba lakini mama mkwe wangu hakuweza kuonekana akiwa
hai ama amekufa,” anasema Steven Francis.
Francis anasema baada ya kushindwa walikwenda kwa
majirani kuomba msaada wa kumtafuta; walikwenda kwa jirani Selis Silili
na Calist Step
No comments:
Post a Comment