Monday, 27 January 2014
HIZI NI DALILI ZA MSICHANA MWENYE MAPENZI KWA MWANAUME JAPO HAWEZI KUSEMA
1 KUONGEA NA KUKAA MUDA MWINGI NA WEWE
kama msichana anakupenda hatoichezea nafasi ya kukuona kukaa na kuongea na wewe. Siku zote atatafuta nafasi ya kuongea au kukuona. Unapoongea naye anakuwa makini kukusikiliza na hufurahi kila unachokiongea hata kama hakifurahisha.
2 ATAKUPA MAWASILIANO YAKE
hawezi kukunyima namba ya simu kwa mara ya kwanza hata kama ni siku ya kwanza mmeonana.
3 ATAKUTAMBULISHA KWA NDUGU NA RAFIKI ZAKE
hajali wengine wakimtazama wanapomuona yu na wewe. Atakutambulisha kwao bila kujali chochote.
4 Wivu
anajisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Unachart nao ukiwaita majina ya kimahaba.
5 ATAKUMBUKA SIKU ZAKO MUHIMU
atajitahidi kukumbuka siku yako ya kuzaliwa na hata akakuletea zawadi. Akisha gundua kitu cha pekee ulichokuwa ukikitarajia umekifanikisha kama kufaulu mtihani haraka sana atajitahidi kukupongeza.
5 MAENDELEO YA BAADAYE
hupenda kuongelea maendeleo yake ya baadaye na kukujumuisha katika hayo. Yupo tayari hata kukushirikisha katika ndoto zake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment