Kufanya
kazi sehemu moja au kuzungumza na mwanamke mwenye mvuto kunaweza kumfanya
mwanaume apoteze umakini wake, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na
Jarida la New Study.
Wanaume
wanaofanya kazi kwenye makampuni yenye ‘visura’ wengi, ufanisi wao ni wa
kiwango cha chini kulinganisha na wasiokuwa kwenye mazingira hayo, sehemu ya
utafiti inaeleza.
Sababu
ya kuwepo kwa hali hiyo ni uchunguzi kubaini kuwa, akili za wanaume wenye
kuvutwa na sura wakati wakifanya mambo hukabiliwa na mgongano wa hisia mbili,
za kazi na mapenzi.
Kuwepo
kwa vitu hivyo viwili kwa wakati mmoja ndani ya akili ya mwanaume, utafiti wa
kitaalamu uliochapishwa na Jarida la Journal of Experimental and Social
Psychology, umebaini kuwa mwanaume ana hatari kubwa ya kufanya vibaya kikazi
kwa sababu wakati akifanya kazi yake atakuwa pia akifanya kaziya kushawishi au
kuimarisha hadhi yake mbele ya mwanamke aliyemvutia.
Ukichunguza,
utabaini kuwa, tabia za wanaume (si wote) hubadilika pindi wanapokuwa mbele ya
wanawake warembo, hii ikiwa na maana kuwa, kama mwanaume ni mwenye maneno mengi
na mpayukaji kwa mfano, hujikuta akilazimika kushusha sauti yake, kuongea kwa
unyeyekevu na busara lengo ni kutaka kumvutia msichana.
Hali
hiyo inapojitokeza ndiyo inayotajwa kudhorotesha umakini wa mtu na kumfanya
afanye kazi zake kama ‘msanii’ anayeigiza na hivyo kuathiri utendakazi wake.
Wakati
nafanya uchunguzi wangu kwa kuoanisha na ule wa watafiti wengine wa kimatafa
ukiwemo wa Dr. Irva Hertz-Picciotto, kutoka Chuo cha Carifonia Marekani,
nilibaini pia viashiria vingine vya ufanisi duni wa kimasomo kutoka shule za
jinsia moja na zile za mchanganyiko, ambapo uchunguzi unaonyesha kuwa wavulana
wanaosoma shule huku wakiwa na uhusiano wa karibu na wasichana warembo
huathirika kisaikolojia.
Hata
hivyo, upo ushahidi mwingine kwamba kiwango cha kufaulu cha shule mchanganyiko
kuwa chini kuliko wa shule za wasichana au wavulana peke yao, katika
kulithibitisha hili mazingira ya shule na malezi yanazingatiwa.
Katika
kumbukumbu iliyowashangaza wanasaikolojia na watafiti wa chuo cha Radboud cha Netherland
ni pale mmoja wao aliposhindwa kukumbuka na kumwelekeza msichana mwenye mvuto
aliyekutanishwa naye ramani ya eneo analoishi, jambo ambalo wenzake walisema
lilitokea kwa sababu alikuwa kwenye mhemko wa hisia za kimapenzi.
Utafiti
wao huo ulihusisha pia watu wengine na matokeo yalionyesha udhaifu mwingi kwa
wanaume, huku wanawake wakiwa na kiwango kidogo cha kuathirika kwa kukutanishwa
na wavulana wenye mvuto.
Ingawa
si jambo la hatari sana kufikia hatua ya kulitangaza moja kwa moja kuwa ushirikishwaji
wa wanaume na wanawake warembo katika ofisi, masomo na kazi mbali mbali una
madhara lakini kitaalamu imebainika kuwa ni vema kundi linaloathirika ambalo ni
sawa na asilimia 19 ya wanaume wote likapewa elimu ili kupunguza zaidi madhara
ya kisaikolojia.
Changamoto
hii, inamtaka kila mwanaume kupima mwenyewe mhemko wa nguvu za warembo kwa
kujiuliza maswali ambayo yatamuwezesha kujua kama yuko kwenye kundi la wanaume
wanaoweza kuathirika kisaikolojia kwa kufanya kazi na wanawake wenye mvuto au
la! Lengo likiwa ni kuchukua hatua za kujikinga na madhara ya kisaikolojia.
Mwanasaikolojia
Dr George Fieldman anakumbusha kitu muhimu alichokipa jina la ‘Reproductively
Focused’ kuwa ndiyo sumu kali inayowadhuru wanaume wengi wanapokutana au
kukutanishwa na wanawake wenye mvuto. Inaelezwa kuwa wanaume wanaovamiwa haraka
na hisia za kimapenzi ndiyo wanaoweza kupata madhara ninayoyaeleza kwa kiwango
kikubwa.
Zipo
njia nyingi za kitaalamu za kupima ili kubaini kuwa mwanaume anakabiliwa na
tatizo hili au la! Lakini pamoja nazo ni hii ya kujibu maswali, ambayo
imeonekana kuwa ni rahisi zaidi kwani haihitaji mtaalamu wa kumuongoza mhusika
bali ni kwa mtu mwenyewe kutafakari na kupata majibu kama urembo wa mwanamke
unaweza kumuathiri kiutendaji. Maswali ya kujiuliza ni haya:
>>Je una uwezo wa kuongea na mwanamke bila kushika shika vitu? Kwa mfano kuingiza mikono mfukoni, kuchezea simu, kalamu au hata kujipapasa mwenyewe.
>>Je Unaweza kutazamana naye usoni kwa zaidi ya sekunde 36 bila kuona aibu? Unaweza kutembea hatua nne mbele ya mwanamke bila kuhisi mwili wako ni mzito?
>>Je unajiamini unapokuwa na mazungumzo na mwanamke hasa mkiwa wawili tu, au mpaka uwe na mtu mwingine?
>>Je umewahi kuwa na ukaribu na wanawake warembo wangapi na kati yao ni wangapi uliwatongoza?
Baada
ya kujiuza maswali hayo sahihisha kulingana na majibu yako. Endapo utakosa yote
fahamu kuwa wewe ni miongoni mwa watu wanaoweza kupata athari ukipewa nafasi ya
kufanya kazi na wanawake warembo. Kumbuka kuwa jibu la mwisho lazima idadi yake
isizidi nusu, endapo umewahi kuwa na urafiki wa karibu na wanawake warembo 10
kwa mfano na kati ya hao watano au zaidi uliwatongoza, utambue kuwa
unaviashiria vibaya vya kupata
madhara tunayoyazungumza.
madhara tunayoyazungumza.
Ifahamike
pia kwamba watu wanaotafunwa na ‘virusi’ hivyo vinavyoletwa na mvuto wa
wanawake warembo ndiyo hao ambao hutumia vyeo au nafasi zao vibaya kwa kuajiri
au kutoa nafasi za
upendeleo kazini kwa wanawake wasiokuwa na sifa za kufanya kazi husika na hivyo kujikuta ofisi, wizara na hata biashara zinakosa tija.
upendeleo kazini kwa wanawake wasiokuwa na sifa za kufanya kazi husika na hivyo kujikuta ofisi, wizara na hata biashara zinakosa tija.
Wakati
nafanya uchunguzi kuhusu tatizo la kushirikiana kikazi na wanawake warembo
ambapo niliwahoji baadhi wanafunzi, wafanyakazi na wafanyabiashara maswali
niliyoandika hapo juu, wengi walibainika kuwa na tatizo hili, hata hivyo changamoto
iliyokuwepo ni juu ya swali lao la msingi kwamba wafanye nini wasiathiriliwe
kisaikolojia baada ya kuwepo kwa dalili za tatizo?
Jibu la swali hili ni dogo nalo ni kujitambua na kuwa makini.
Jibu la swali hili ni dogo nalo ni kujitambua na kuwa makini.
Inashauriwa
kuwa watu wenye matatizo haya wanatakiwa kudhibiti mawazo yao ya kimapenzi mara
wakutanapo na wanawake warembo na kusimamia vitu halisi. Jambo la mwisho ni
kujiamini na kutenda yale wanayofahamu.
Katika
hali ya kawaida tatizo la mvuto wa wanawake hugusa zaidi hisia, hivyo mara
nyingine ni vigumu kwa mtu kuweza kuzuia msukumo usitokee, lakini kwa
aliyejitambua itakuwa rahisi kwake kutoendeleza mawazo ya kimapenzi sambamba na
kazi.
Wakati
mwingine ni suala la mtu mwenyewe kuamua kusimamia kazi na kupuuza hisia za
kimapenzi zilizotokana na mvuto wa mwanamke mrembo, kwa vile si lazima kila
mawazo au hisia zinazotokea ziendelezwe.
Hebu
tujiulize ni mara ngapi huwa tunawaza au kuhisi vibaya na tukaacha kufanya kama
tulivyofikiri kabla? Je hakuna vipindi ambavyo huwa tunawaza kuua, kuacha wake
zetu na hata kufanya mapenzi na ndugu na mambo mabaya kama hayo na tukayapuuza
mawazo hayo? Ikiwa tumeshafanya hivyo tufahamu kuwa nguvu kubwa iko kwenye
uamuzi wetu.
Nikimalizia
somo hili ni kwamba, mara nyingi wanaume wenye aibu na hofu mbele ya wanawake
ni wale wanaodhani kuwa wanakasoro fulani ambazo zinaweza kuwakosesha penzi na
hivyo kuamua kujikarabati kwa unyenyekevu, sauti za chini, hongo, kutembea kwa
madaha na wakati mwingine kujifanya ni watu wa tofauti sana kwenye jamii, jambo
ambalo huweza kuathiri mwenendo wao na kuwa watu wa kuigiza igiza mambo
yasiyoendana na uwezo wao halisi au kile wanachokifahamu.
Nimalizie mada hii kwa kufafanua kuwa lengo la makala haya si kuzuia ushirika kati ya wanaume na wanawake warembo bali kufundisha watu kuhusu madhara yake ili ukiwapo urafiki uwe ni ule wenye tija, usioathiri ufanisi wa kazi.
KUMBUKA;
ingawa somo hili linawahusu zaidi wanaume lakini kwa upande mwingine linawagusa
wanawake ambao hufanya kazi na wanaume watanashati na wenye mvuto.
No comments:
Post a Comment