msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, walio
makini kwenye
WAPENDA USAWA
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa
kimapenzi ni
wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba
majukumu ya
kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa
kuongoza jamii
kwa asilimia 50 kwa 50
WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa
yao kubwa ni
uwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa.
Tafiti zinaonesha
kuwa wanaume hupenda
sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa
sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za
wanaume
bila kujali sifa zao za nje au za ndani
MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne
inayowavutia wanaume.
Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna
wanavyojali
na kujitolea
kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na
raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda
amani
WAPENDA UWAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye
msimamo na
wapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya
msingi kwa
kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake
wa aina hii
wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na
udhaifu katika
uelewa wa mambo.
WANAOJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti
na akina
‘naomba vocha’ kila siku. Uchunguzi
unaonesha kuwa wanaume wa leo
hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na
wanaoendekeza starehe
za upande mmoja.
WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha
wasiolazimisha vitu
vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee
yenyewe na
kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi
MARIDADI
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni
wanaozingatia usafi
na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto
wa nje lakini
pia ni waelewa wa
mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano.
WANAORIDHIKA
Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio
kikubwa kwa
wanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu
wa mapenzi
kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa
yakiwageuza kutoka
juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila
kubadili tabia ni
sifa njema ya
mwanamke
WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari
kukwepa kila
aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana
vitu vya ziada
zaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana.
“Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki
mtu mwingine.”
Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana
No comments:
Post a Comment