Harare.
Kiongozi wa kanisa moja nchini Zimbabwe amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa kosa la kuwabaka wanawake watatu na kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana.
Kiongozi huyo, Martin Gumbura (57) wa Kanisa la
RMG Independent End Time Message alitiwa hatiana katika makosa manne ya
ubakaji kwenye mahakama ya mjini Harare. Gumbura ana wake 11 na watoto
30 na aliiambia mahakama kwamba alikuwa akitarajia kupata watoto 100
katika maisha yake.
Wake zake wote walikuwa wakihudhuria mahakamani
hapo wakati wa kesi hiyo na walikuwa wakijumuika na watu wengine
waliokuwa wakihudhuria makahamani hapo hadi siku hukumu ilipotolewa.
Alihukimiwa kifungo cha mika 50 jela lakini miaka
10 imepungizwa katika adhabu hiyo baada ya kuonyesha tabia njema wakati
wa kesi hiyo.
Hukumu nyingine ya kifungo cha miaka minne jela
kwa kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana itatumikiwa sambamba na
hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 40. Waendesha mashtaka waliiomba
mahakama kwamba Gumburu anatakiwa ahukumiwe kifungo cha miaka 25 jela
kwa kila kosa, lakini hakimu alieleza kwamba hana mamlaka ya kutoa
hukumu ya kifungo cha muda mrefu namna hiyo.
Hakimu huyo alimwelezea Gumbura kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo ambaye amekuwa akiwaghilibu waumini wa Kanisa hilo.
“Mahakama imejaribu kutoa adhabu ambayo
itawatendea haki wote, malalmikiwa na walalamikaji. Mtuhumiwa hutu ni
kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo,” alisema.
“Msingi wa huduma ya Kanisa ni kumwabudu Mungu na
si kuzini na mabinti na wanawake na kuwatishia kwamba kwa kutofanya
hivyo watapatwa na balaa,” aliongeza hakimu huyo.
Alisema ni wajibu wa wachungaji na wasimamizi wa
kanisa kujua kuhusu madhila yanayowakumba waumini wao, pia kujua
udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia unaowakumba wanawake na
kutafuta namna ya kuukemea.
Awali Gumbura alikuwa akikabilwia na mashtaka tisa
ya kuwalaghai na kuwabaka wanawake sita lakini alifutiwa mashtaka manne
yaliyowahusisha wanawake watatu kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa
kutosha.
Hivi karibuni, mtu mwingine mjini Harare
alihukumiwa kifungo cha miaka 290 jela kwa kosa la kuwadhalilisha na
kuwabaka wanawake 13. Mtu huyo, Thomas Chirembwe (30) alitiwa hatiani
kwa makosa 21 ya ubakaji na ujambazi wa kutumia silaha baada ya
mfululizo wa matukio yaliyoutikisa mji wa Harare.
Kwa mujibu wa takwimu za polisi, zaidi ta watoto
400 walibakwa na wanawake 392 walinyanyaswa kijinsia mwaka 2013, ambapo
wanawake walibakwa wakiwa njiani na watoto wengi walibakwa na majirani
au watu wao wa karibu.
No comments:
Post a Comment