SUPER STAR JOKATE ALIVYOMSHANGAZA WEMA SEPETU ARUSHA LIVE ONA ALICHOFANYA!!
Unaweza
kujikuta ukishindwa kuielewa hii hali lakini inabidi ukubaliane na
ukweli halisi wa hiki kilichotokea,Jokate na Wema historia yao ilianzia
kwenye shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2006 ambapo Mshindi alikua ni
Wema Sepetu akifatiwa na Jokate kisha mshindi wa tatu akiwa Lissa
Jensen. Headline
zilikuja kutengenezwa tena zikiwahusisha warembo hawa kuonekana wako na
mtu mmoja ambapo magazeti mengi yaliandika mahusiano haya yaliyokua
yakimhusu Diamond Platnumz kutoka na warembo hawa. Kimepita
kimya kirefu sana juu ya hawa watu wawili hadi usiku wa February 01
huko Arusha kwenye Tamasha la Divaz Night Endless Fame ambalo ndani yake
kulikua na mastar kadhaa akiwemo Wema Sepetu,Aunt Ezekiel,Martin
Kadinda,Kajala,Zamaradi Mketema,Chid Benzi,Mirror,Jordan na wengine
kibao. Wakati
Madam Wema Sepetu akimwaga mauno kwenye jukwaa bila kutegemewa na mtu
yoyote Jokate alipanda Jukwaani na kuanza kumtunza Wema pesa na wakati
huo Wema alikua akicheza Wimbo wa Diamond My Number One ‘Ngololo’ ambapo
Jokate aliungana na Wema kuucheza Wimbo huo.
No comments:
Post a Comment