Namna mdomo unavyoharibika kutokana na ngono kufanywa kwa kutumia mdomo.
- Baadhi ya watu ambao wanakumbwa na ugonjwa huu shingo huvimba kama hivi. Hata hivyo wapo wenye kuvimba hivi lakini si kwa sababu walifanya ngono kwa kutumia mdomo, isipokuwa yaweza kuwa ni sababu nyingine zikiwemo kurithi.
- Wataalamu wa masuala ya afya wanashauri kwamba ni muhimu sana watu wakaachana kabisa na tabia hii kutokana na ukweli kwamba siyo tu kwamba ni hatari kwa afya, pia ni sawa na kujiua mwenyewe, kwani kitendo hicho kinachangia magonjwa mengi.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani
(WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na
ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”.
Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,
pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana
wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo
hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini
wanaume 747 na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na
saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444
wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana
wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza
wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi wao katika
kushiriki ngono.
Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa
sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi
wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe
wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi
hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau
wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana
kama ni chafu pia.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani
ya koo ni ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume
nchini, ikiongozwa na ile ya ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo
huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24
zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya
watu hupata saratani ya koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na
wengine kuwa na umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini
siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.
“Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya
wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini
mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze
kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili
hii haikuwepo kabisa,” anasema Dk Kahesa na kuongeza.
“Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
“Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
No comments:
Post a Comment