Wednesday, 24 April 2013

Diamond azidi kumdhalilisha Wema..


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond na vimwana vyake..

WAKATI msanii wa filamu nchini Wema Sepetu akilia usiku na mchana juu ya kitendo alichofanyiwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Nassib Abdul (Diamond Platinum) za kumrekodi na kusambaza sauti yake kwenye mitandao, Platinum amejitokeza adharani na kukiri kuhusika.
Wema na Diamond wamewahi kuwa na mahusiano ya  mapenzi kwa kipindi kirefu na hatimaye kumwagana huku mwanadada huyo akiwa bado mwenye mahaba mazito.
“Wema amekuwa akinipakazia mbovu kwa mpenzi wangu Penny akiwa na lengo la kuharibu mapenzi yetu, nilichukia sana na siku alipoamua kunipigia simu ndipo nikaamua kumrekodi ili kumsikilizisha Penny ambaye alikuwa haniamini kabisa” alisema Diamond kwa madaha.
"Alikuwa akini bembeleza ili turudiane kwa sababu bado ananipenda, nilazima nikiri kwamba nilimrekodi lakini lengo ilikuwa ni kulinda penzi langu ambayo ilikuwa hatarini kuvunjika kwa sababu yake"alifafanua Platinum.
“Hata hivyo lengo langu haikuwa kuiweka mitandaoni ili watu wajue bali kumsikilizisha mpenzi wangu Penny, na ilipofika mitaani sikufurahia ila sikuwa na jinsi kwa sababu tayari ilisha fahamika".
Msanii huyo alipotakiwa kumwomba mwanadada huyo msamaha hadharani kupitia vipindi vya redio na TV pamoja na mitandao ya jamii ili wamalize bifu jemba hilo likagoma na kudai kwamba hawezi kumwomba msamaha.



Kitendo hicho kiliwahi kumfanya Wema kuandika maneno makali yaliyojaa dalili za kukata tamaa ya kusihi kwenye mitandao ya kijamii, huku akidai kwamba siku akifa lazima kuna watu watahuzunika sana.
"Najua hivi sasa hakuna anayeweza kutambua umuhimu wangu katika hii duniani, ila nina amini kwamba siku nitakapoiaga dunia na kuwacha peke yenu ndipo mtakapotambua umuhimu wangu kwenu"alisema Wema katika mitandao ya kijamii.
Wema Sepetu ni kati warembo mahiri na wenye kila sifa ya kuwa mke wa mtu mmoja mwenye hehma zote za kuwa mume wa binti kama yeye, lakini binti huyo amekosa bahati huku akikumbwa na mikasa ya mapenzi kila wakati.

No comments:

Post a Comment