AINA KUMI YA VYAKULA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KUFANYA MAPENZI KWA WANAUME:
Mahaba
pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume
na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi
umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja
kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo,
watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya
vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la
ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:
PILIPILI
Pilipili
zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji
damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa
na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale
wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si
kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.
PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya
tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha
vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa
watu wanaotumia tunda hili kwa
wingi huwana msisimko mkali wa
kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye
utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa
kujamiiana.
NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema
tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo
inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa
msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini
na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.
CHOKOLETI
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na hivyo kumuwezesha mtu
anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake,
jambo litakalomuwezes ha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya
mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa
mawazo.
CHAZA NA PWEZA
Aina hizi za samaki zinazovuliwa
baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia
uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo
la ndoa.
POMEGRANATE
Ni aina fulani ya matunda mekundu
yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu
na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo
kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.
MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na
kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na
baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao
wanasumbuliwa na
tatizo la kushindwa kurudia tendo.
MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga
husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya
njema.
VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI
MAJI ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa.
No comments:
Post a Comment