Kwa kawaida Wanawake tunadondoka kimapenzi haraka zaidi kuliko wenzetu.
Huenda Mwanaume akawa amevutiwa na Muonekano wako, Uzuri, Uwezo kiakili,
Sauti, Utembeavyo n.k. Mkaanza au mkakubaliana kutoka kama wapenzi.
Hiyo hamfanyi yeye kukupenda wewe!
Enzi za Bibi yangu ilikuwa ni kawaida kwa Binti kuolewa bila kumpenda
Mwanaume, kwamba kila kitu kinatayarishwa na familia mbili na wewe kama
Binti unaambiwa tu utaolewa na Bwana fulani Mtoto wa Familia/Ukoo
fulani.
Kabla ya kuchumbiwa Binti unakuwa tayari umefundwa kuhusianana mambo
mengi tu kuhusu Mapenzi, Ndoa, Uzazi na Mabadiliko yatakayoendelea
kujitokeza kwenye maisha yenu kama Wazazi na Wapenzi.
Ikiwa kwa bahati nzuri unamfahamu “Mchumba” na pengine ulikuwa
unapendezwa nae basi unahitaji kumfanya akupende(baada ya ndoa) na ikiwa
bahati akakupenda ghafla basi unapaswa kumfanya akupende zaidi, yaani
umkae moyoni na kichwani(akilini).
Kipindi hicho Wanaume wengi walikuwa wanafunga Ndoa ili kuendeleza
Ukoo(kuzaa) na kujiwekea heshima kwenye Jamii sio kwa mapenzi kama
ilivyo sasa kwa baadhi yetu. Wachache sana walifunga Ndoa kwa vile
waliwapenda Wanawake waliochaguliwa.
Hii bado inaendelea hadi sasa kwa baadhi ya wanaume wa “kisasa” na
Wasomi, kwamba “anatafuta” Mke ili amzalie watoto na kuwalea, ampikie na
kufanya shughuli zote za ndani.
**Kutokana na “Maendeleo” au sijui ni mambo ya Usawa siku hizi nasikia
kuna Wanawake wanafunga Ndoa kwa sababu nyingine na sio mapenzi (hii ni
topic nyingine).....tumalizie hii kwanza.
Changamoto:
Kutoa changamoto ni tofauti kabisa na kutokuwa msikivu au kutokuwa na
heshima kwake. Wanaume hawakuzaliwa wakiwa wanajua kila kitu na ndio
maana tukaumbwa sisi kama wasaidizi wao, kwamba kuna wakati wanahitaji
kuwekwa sawa kiakili, kiutendaji(kitandani included), Sio kila asemacho
wewe ni "ndio Bwana" hata kwenye suala ambalo halihitaji "ndio".
Mapishi:
Ukiachilia mbali suala la Kuridhishana na kufurahisha Mwili, kujua
kupika aina mbali mbali za vyakula ni muhimu pia. Unapofundwa unaambiwa “
kamwe usiruhusu Mpenzi wako kula chakula cha mwanamke mwingine hata
kama dada ni dada yake.
Kwa kawaida Wanaume wengi husifia na kupenda mapishi ya mama zao, sasa
hapa ndio muhimu kujenga uhusiano mzuri na Mama mkwe nakuhakikisha
unajifunza ili ukampikie mwanae nyumbani kwako.
Usafi wa nguo:
Najua wanawake wengi wa “kisasa” wanapinga sana hili lakini sie
tuliofundwa na wa kisasa tunachanganya yote ili “kushinda”
hihihihi....Kamwe usivundike nguo mpaka anaishiwa ya kuvaa, ni vema
kuhakikisha nguo ni safi na zimenyooshwa vyema.
Maendeleo:
Hata kama huna kipato sio mbaya kuchangia maendeleo kwa kutoa mawazo
mazuri na endelevu, na hata kuchangia katika utafutaji wa “info”
kuhusiana na mfano Ujenzi, upatikanaji wa Mbegu za mazao fulani au
Bidhaa kwa ajili ya mradi fulani n.k.
Kujali:
Zamani hakukuwa na urahisi wa mawasiliano hivyo ilikuwa muhimu kumpokea
mpenzi na kumpa pole, kumkumbatia anapofika nyumbani, unakaa nae na
kuulizia hali yake na siku ilivyokwenda.
Siku hizi ni rahisi kimawasiliano hivyo basi sio mbaya kama utaulizia
anavyoendelea huko aliko....ni mpenzi wako tayari hivyo huwezi kuonekana
“needy” ikiwa uta-check anaendeleaje akiwa kwenye mishughuliko yake
badala ya kusubiri yeye ndio akupigie au akutumie ujumbe.
Jipende Kimwili:
Enzi zile ilikuwa ni Usafi, valia Khanga Mbili na kujifukiza
Udi....inategema na ufanyacho ili kujipenda kimwili(kuvaa vizuri, kunyoa
vinyweleo, kufanya mazoezi, n.k) aili mradi tu kinakufanya ujisikie
vizuri na kukuongezea hali ya kujiamini na kuwa tayari kwa
lolote(namaanisha Tendo)....siol azimalitokee lakini pia sio mbaya kama
ukiwa tayari wakati wote.
Tunza Haiba ya Uanamke wako:
Pamoja na usomi wako au kuishi kwako sana na Wazungu, usisahau kuwa wewe
ni mwanamke wa Kiafrika kwenye maadili (inategemea na kabila) fulani
ambayo hao wa “kisasa” hawana na hiyo inakufanya wewe uwe tofauti na
wanawake wengine wengi Duniani.
Pamoja na kusema hivyo haina maana uvumilie unyanyaswaji kwa vile tu
kikwenu kunyanyaswa ni sehemu ya Maadili, chukua maadili mazuri na yenye
manufaa kwako na kwa mpenzi wako.
Jitegemee:
Hupaswi kusubiri yeye afanye manunuzi fulani bali wewe kama mwanamke
mwenye kipato unapaswa kuangalia nini kinahitajika/kosekana ndani na
kurekebisha mambo. Natambua baadhi ya wanawake wenye kipato lakini
hutegemea wanaume wawafanyie kila kitu wakiamini kuwa kufanya hivyo
kutamzuia mwanaume huyo kuhonga nje ya uhusiano wake.
Unapoonyesha kuwa unajitegemea unamjengea mpenzi wako imani kuwa hata
mkiwa na watoto na yeyekupoteza kipato au hata kufa wewe kama mwanamke
utaweza kutunza watotowenu bila tatizo lolote. Ikiwa huna kipato basi
sio mbaya kama utakuwa unamkumbusha mpenzi pale panapokuwa na mapungufu
ya vitu ndani ya nyumba yenu.
Kidokezo: Vitu vidogo kwenye ambavyo pengine wewe unadhani havina umuhimu ndio hivyo hivyo vinavyoweza kuharibu uhusiano wenu.
Mf: Nguo zote chafu hivyo inabidi avae nguo ambayo haipendi na hivyo
kuwa “uncomfortable” huko kazini, ikiwa kachekwa ni wazi hatokuwa na
furaha hata akirudi nyumbani na hali hiyo ikiendelea ni wazi kuwa
uhusiano wenu utakuwa Mashakani.
Ahsante kwa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment