Sina hakika ni kwanini wenzetu (wanaume) wanapenda Matiti wakati sisi
(wanauwake) ndio tunaonyegeka ikiwa yatafanyiwa "kazi" vizuri na kwa
utaalam. Ukiachilia mbali hilo, matiti hutufanya tuhisi kuwa ni
"wanawake" pia ni Mwanzo mzuri wa maisha ya mtoto).
Nakumbuka mara ya kwanza kuvaa Sidiria ilikuwa 2003, sikuwa nahitaji
lakini nilidhani kuwa kuvaa Sidilia ndio "uanamke", basi nikaenda kupima
size ya Matiti ili kupata "Bra" itakayonitosha vema. Wahudumu
wakanishangaa na kusema kuwa ninge-save pesa nyingi kwa kutovaa "Bra"
kwani sihitaji, lakini kwa vile nilitaka kujihisi kuwa ni mwanamke
nilisisitiza kupata "Bra" yangu ya kwanza....TMI i know, sorry
hihihihi....
Katika hali halisi hakuna Mwanaume anaependa kukutana na mwanamke ambae
matiti tayari yapo tumboni (inategemea na ukubwa), hiyo haimfanyi
mwanaume huyo kuchukia matiti yaliyoanguka ila angependa yaanguke akiwa
Mkewe na sababu iwe ni kunyonyesha watoto wao.
Hebu badilishakibao wewe ndio uwe mwanaume etii....alafu unakutana na na
titi zipo tumboni, hapo hajanyonyesha/Zaa, utakuwa hujui raha ya
matiti yaliyosimama na pengine siku moja ungependa kupata uzoefu
huo....Hebu fikiri.
Kwa bahati mbaya wanawake wengi kwenye jamii rejea topic ya Jinsi ya
kutunza, wengi hujiachia tu kipindi ambacho matiti hayo yanahitaji
"support". Hakika Matiti kuanguka ni kutokana na kunyonyesha watoto wa
Mumeo, lakini kumbuka kuwa sio Wanawake wote wenye matiti yaliyoanguka
wamenyonyesha, Wamezaa, Wametoa mimba au wanawaume/wapenzi....kwamba
matiti yao yalianguka kitambo kabla hawajanyonyesha kutokana na
kutoyatunza vema.
Ikiwa mumeo alikukuta ukiwa na matiti Saa sita bila shaka ataendelea
kuyapenda akijua kuwa wanae waliyatumia "early days of their lives",
obviously atakuwa amekubali mabadiliko uyapatayo kutokana na
Uzazi....lakini at least aliyakuta Wima na yeye ndio kachangia yatazame
Chini (baada ya kunyonyesha watoto).
Ukweli wenye maumivu ni kuwa, Asilimia kubwa ya wanaume wangependa
matiti ya wake zao au wapenzi wao yadondoke wakiwa nao na sio wayakute
yakiwa hivyo (matiti yamedondoka). Hali inayofanya wengi wao kuzungumzia
u-wima wa matiti na kucheka au kubatiza yale yaliyolala kuwa ni Malapa.
Mimi binafsi huwa sipendezwi na hilo na siku zote huwa nasema kabla
hujamcheka mwanamke mwenye matiti yaliyolala hakikisha wanawake kwenye
familia yako bado matiti yao yapo wima na muhimu kabisa ni je Matiti ya
mama yako uliyonyonya bado yamesimama(saa sita)?
Ikiwa kwa bahati mbaya wewe ulichelewa ama ulikuwa hujui namna ya
kutunza matiti wakati yananza kujitokeza hakikisha Wanao wa kike
wanajua(wafundishe), pia hakikisha unayapa "support" yakutosha
unapofanya Mazoezi, Unapo karibia hedhi, unapokuwa Hedhini, utakapo kuwa
Mjamzito na wakati unanyonyesha.
No comments:
Post a Comment