1. KUWA MUWAZI kama upo tayari kuongea na ex wako mkikutana, akuulizapo
swali lolote mjibu inavyotakiwa kwa majibu mafupi yasiyo ya kubabaisha
yenye ukweli mtupu. Kama ni ndiyo 'ndiyo' na kama ni hapana 'hapana'
itakufanya kujenga utu wako na kukupa kujiamini.
2. USIJITONGOZESHE kama umeshaachana na mpenzi wako mpya kwa sababu
ya huyo mpenzi wako wa zamani usifanye mambo ya kujitongozesha kama
vile kukaa naye karibu kumchekea chekea au kumtega kwa namna yeyote ile
kama ikitokea bado unampenda muache yeye akuanze na umsumbue katika
kumjibu kwa sababu kama mlishaachana huna hakika lile kosa halitajirudia
mkirudiana.
3. KUWA NA MAWAZO CHANYA wengi wanapokuwa pamoja
na wapenzi wao waliopita hufikiria negative hujiuliza anawaza nini?
Ananiona mbaya? Vipi kama anakuja kunionesha mpenzi wake mpya? Haya ni
maswali machache yanayowapitia wengi vichwani mwao. Lakini kama ukiwa na
mawazo chanaya unaweza kujiamini na uwezo hata wa kumface huyo mpenzi
wako aliyepita kwa hiyo uwapo na ex wako fikiria mawazo chanya.
4.RELAX muda mwingi watu mnapokutana na wapenzi wenu waliopita huwa
mnapanic kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kutulia na kuvuta hewa nyingi
ndani na kutoa nje hii hujenga kujiamini na kuondoa hofu iliyojengeka
usoni mwako
5. USIONESHE KUKOSA FURAHA KATIKA PENZI LAKO LA SASA
usimpe nafasi x wako kujiona yeye ni muhimu sana katika maisha yako
yaani ajione yeye alikuwa ni furaha yako ya pekee hata kama huyu wa sasa
hana tofauti na yeye lakini jitahidi kujiweka sawa na kumuonehsa kuwa
hakuna tatizo huyu wa zamani ili kujenga kujiamini kwako kila
mnapozungumzia habari za mahusiano.
No comments:
Post a Comment