Tuesday, 13 August 2013

WALTER CHILAMBO AFUNGUKA BAADA YA NAY WA MITEGO KUMTUHUMU KUWA NI MASIKINI WA KUTUPWA

Baada ya maneno na tuhuma nzito za Ney wa Mitego dhidi ya Mshindi wa Epiq Bongo Star Search mwaka 2012, Walter Chilambo kuwa  huenda  amedhulumiwa zawadi yake ya ushindi, Shilingi Milioni 50 na waratibu wa shindano hilo kwa sababu mpaka sasa yupo katika maisha duni, Msanii huyu amevunja ukimya na kusema kuwa yeye yupo vizuri  kifedha.


Walter amesema kuwa maneno ya  Nay  hayana ukweli wowote na yeye anaishi vizuri na  hadhani kama Nay wa mitego  alikaa chini na kufikiria kabla ya kuongea kuhusiana na issue hii katika wimbo wake, wala hakufanya uchunguzi wowote ambao uliomhusisha yeye.



Walter amemaliza kwa kusema kuwa, Maneno haya hayamuumizi kwa  vile hayana ukweli wowote, na vilevile hayawezi kumuondolea mashabiki wake.

No comments:

Post a Comment