Monday, 21 October 2013

ADHABU KUBWA YA MPENZI ANAYEKUSALITI


 Wanaume wengi wanapobaini kuwa wapenzi wao wanawasaliti, hutunisha misuli kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa wana mapenzi unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.

 Kuna wengi ambao waliwafumania wake zao, wakawapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana kwa maneno haya: “mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi Wapendanao Gesti” au “vipi yule bwege alikuuliza jana ulipochelewa kurudi” Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenzi wa mtu.

 Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana mume/mke. Watu huazimana magari na pesa, lakini laazizi hakuna jasiri wa namna hiyo! Hivyo ndivyo lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia? Jibu hakusaidii, kwani ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo,  kesho yake watakaokutana watakusaliti tena kupozana machungu.

 Maamuzi ya kuacha naye hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona wameshikana mikono mitaani kwa uhuru na raha zao.

 Ukiamua kuua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila siku, si tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?

 Hivyo, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali akibembelezana na ‘kidume’ mwingine kwa maeneo  fulani. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa umeona lile la stejini laivuuuuuu bila chenga. Twende pamoja ili tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi msaliti.

 Kwanza, baada ya kuwaona uso kwa macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa umewaona, halafu ondoka eneo hilo. Ukifika home mtu mzima endelea kunywa maji ili kupoza presha. Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha, lakini usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe.

 Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza, kisha baada ya kumaliza uchunguzi wako mtumie tena sms hizo mkeo/mumeo. Ukifanya hivyo usimuulize, endelea kumpenda na ikiwezekana ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’ akaange kila siku na umpe penzi moto moto.

 Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache! Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!

Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu msaliti. Mwadhibu kwa upole, wanasaikolojia wameithibitisha adhabu hii kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya kupiga au kukemea. Ukisema umwache siyo dawa kwani unaweza kutafuta mwanamke/mwanaume mwingine naye akawa na tabia zile zile, ikiwa ndivyo utaacha wangapi basi katika maisha haya?

 Adhabu ya mpenzi anayekusaliti ni kumnasa kwenye usaliti wake kisha kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia kupunguza maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi hakusaidii. 








No comments:

Post a Comment