KWA WANAWAKE: HIZI NDIZO MBINU ZA KUMTEKA AKILI MWANAUME WAKO..HAKUNA HAJA YA KUMWEKEA LIMBWATA..
WANAWAKE
wengi wanashindwa kujua wao wanatofautiana na wanaume kwa hisia na hata
mawazo ya mapenzi. Wanaume wana mambo wanayoyapenda kutoka kwa wake zao
hasa katika masuala ya mapenzi. Kwanza wanawake wajue wanaume wengi
wana hisia za haraka za kufanya mapenzi kuliko wanawake.
Mwanaume
alivyoumbwa ni kwamba akiona tu mfano mwanamke umevaa kanga moja au
umevaa night dress hiyo inatosha kusisimua. Wapo wanawake wanaowasisimua waume zao bila wao kujua. Mfano umevaa tu kanga moja au night dress ndani huna kitu.
Kwako
ni jambo la kawaida lakini kwa mwanaume sio la kawaida kwa kukuona
hivyo tayari unakuwa umeamsha hisia zake. Ukimwona anakuja kutaka haki
yake usidhani anakusumbua. Ujue tayari mwenzako alishafiria mbali zamani
we huna habari.
Ni vyema ukawa mwangalifu kujua hisia za
mwanaume huyo mumeo kama inawezekana mpe anachohitaji kwani usipofanya
hivyo unamwathiri kisaikolojia na anaweza kufikiria nje. Wanawake wengi
wa nje waliowaweka waume zenu kiganjani hiyo ndio mbinu wanayotumia.
Akiwa
na ahadi na mumeo atamkuta kanga moja au amevaa night dress na kila
anachohiji atapewa haraka tena kwa madoido. Kwanini akitaka hayo hayo
kwa mkewe hapewi je ana kosa gani anapofikiria nje?
NB:
Nikisema
mpe mumeo Hitaji lake sina maana Umpe mpaka kinyume na maumbile Ukiona
Mumeo kafikia hapo Huyo Hafai si Mume mwenye Busara huyo na wala
hakutakii mema mkatalie na Umwelimishe madhara ya Tendo la ndoa kinyume
na maumbile.
MVUTIE MUMEO KWA MWENEKANO WAKO. Mvuto
ni muhimu sana kwa mwanaume. Wanaume wanapenda wanawake wanaowavutia
kihisia. Niwaambie wanawake mlioolewa jueni kumvalia mumeo mavazi
yanayomvutia.
Sio
vibaya kama nilivyosema hapo juu ukavaa kanga moja kama upo pamoja nae.
Kama nilivyoeleza hapo juu mwanaume anasisimka kwa kuona. Kwanini
avaliwe kanga moja na wanawake wa nje wakati wewe unaweza kuvaa.
Wanawake
jueni hili mnapokuwa karibu na waume zenu jianchieni Kwa mfano hakuna
ubaya wakati mumeo karudi kutoka kazini akiwa amechoka, wakati
unampotengea chakula ukavaa kanga moja au night dress.
Unaweza
kuona hilo ni jambo dogo lakini kisaikolojia utakuwa umefanya jambo
kubwa. Hapo hata kama atakuwa ameudhiwa kazini atasahau na kukuona wewe
mpenzi wake.
Usafi panga vitu vyako vya chumbani vizuri:
Jambo hili limekuwa lizizungumzwa sana hadi wengine wanasema mwanamke usafi.
Kisaikolojia
mpangalio wa vitu ndani na hasa chumbani kama ni mbovu unaweza kuathiri
hata tendo la ndoa. Kama chumba ni kichafu vitu havijapangwa vizuri
kisaikolojia kunapunguza msisimko wa mapenzi na hata kumfanya mwenzako
achukie kufanya na wewe tendo hilo ukadhani hakupendi.
Mwanamke
tandika kitanda chako vizuri panga chumba chako tandika shuka nzuri.
Siku hizi kuna shuka zina maneno ya mapenzi nunua hiyo uwe unatandika.
Kisaikolojia utamfanya mpenzi wako avutiwe chumba chako na hata wewe
mwenyewe.
Mazingira mazuri yatamfanya asisimke haraka kimapenzi anapokuwa na wewe na hata kuitamana nyumba yake na kurudi mapema nyumbani.
Jinsi chumba kilivyo rafu ndiyo wanasakolojia wanasema kunafanya ubongo uwe rafu hata kuchukia.
Unaweza kumwona mwenzako anachukia kumbe ni kutokana na mpangilio mbovu wa chumba ndio sababu inayomfanya achukie.
Uwe msafi wa mwili:
Sio usafi wa chumba pekee unatosha pia na usafi wa mwili wako ni muhimu.
Niwakumbushe
wanawake hakuna kitu kinachowachukiza wanaume kama mwanamke mchafu.
Asiyejipenda. Sio lazima ujirembe sana lakini jitahidi ukawa msafi. Oga
vizuri paka mafuta au lotion yako jipulizie manukato kidogo yanayomvutia
mumeo.
Sio
lazima utumie gharama kubwa usafi wa kawaida unatosha na kupaka rotion
kuna fanya ngozi ya mwanamke ikawa laini inayovutia wanaume wanapenda
sana wanawake wenye ngozi laini yenye kuvutia inaleta msisimko mumeo
anapokuwa anakuangalia mara kwa mara.
Wanawake wa nje hawana
zaidi ya hayo ni hayo hapo juu na mengine ndiyo wanayotumia kuwaweka
waume zenu kiganjani. Usijaribu kwenda kwa mganga hakuna
atakachokusaidia memeo atatoka kama wewe humsisimui, hupangi vitu vyako
vizuri na pia kama unaendekeza uchafu ni rahisi mumeo kufikiria nje.
Kujiamini
kwako iwe ni kwa sababu unajua ‘kumhendo’ mumeo kwa kumpa mapenzi ya
kiwango cha juu, kumheshimu, mjali na kumpatia mambo ya msingi ambayo
anastahili kuyapata kutoka kwako. Ukifanya hivyo utaifanya roho yake
imsute kila anapotaka kukusaliti.
Hiyo ndiyo iwe sababu ya wewe
kujiamini na wala huna sababu ya kujinadi kwa wenzako. Tambua kuwa kuna
wanaofikia hatua ya kuhatarisha maisha yao kwa kutoa ‘mtandao’ wakijua
kuwa ni njia ya kuwashika waume zao kumbe wanajitafutia matatizo
makubwa.
Wapo waliopoteza fedha zao nyingi kwa kwenda kwa waganga
ili waume zao wasifurukute mbele zao lakini imekuwa kazi bure. Shituka
leo, anza kutumia mbinu sahihi za kuishikilia ndoa yako na usijidanganye
kwa kufanya mambo ambayo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Mwanamke
aliyekamilika ni yule anayeuthamini mwili wake, sasa kwa nini leo hii
ukubali ‘kumrukisha ukuta’ mumeo ili kumfanya asiende nje ? Kwa nini
utumie fedha zako kwenye kumtafutia limbwata mumeo wakati wewe mwenyewe
ni limbwata tosha ?.
No comments:
Post a Comment