Nachingwea. Mtoto mchanga mwenye umri wa siku
mbili amenusurika kufa baada ya mama yake mzazi, Hadija Pangani (29)
Mkazi wa Kijiji cha Mpiruka Wilaya Nachingwea, Lindi kumfunga kwenye
kiroba na kumtumbukiza chooni.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha
Mpiruka, Simon Rashidi alisema mtoto huyo aligunduliwa na Techla Sameul
baada ya kusikia sauti ya kulia alipokuwa anajisaidi kwenye choo hicho.
Simon alisema baada ya kusikia kelele za mtoto
huyo, Techla alitoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya kijiji hicho,
ambao kwa pamoja na kushirikiana na jamii na kufanikiwa kumwokoa mtoto
huyo ambaye alikutwa hai akiwa amezungushiwa gagulo na kufungwa kwenye
kiroba.
Rashidi alisema wakazi wa eneo wakishirikiana na
uongozi wa kijiji walifanya uchunguzi na kubaini kuwa mtoto huyo alikuwa
wa Hadija kwa kuwa alikuwa na ujauzito kwa kipindi hicho. “Tulimfuata
na baada ya kumbana kwa maswali, alikiri kufanya unyama huo kwa madai
kuwa ameelemewa na familia, kwani tayari ana watoto watatu kila mmoja na
baba yake na hakuna hata mmoja anayetoa masaada.
Kamanda wa Polisi Lindi, George Mwakajinga alithibitisha kutokea ka tukio na kwamba mtuhumiwa atafikisha mahakamani.
No comments:
Post a Comment