Vazi la kitenge, ni moja ya mavazi
mashuhuri sana ambalo asili yake ilikuwa ni mwambao wa pwani ya Afrika
ya Mashariki, kabla ya kuanza kusambaa umaarufu wake katika bara zima la
Afrika na hatimaye duniani hivi sasa.
Ni vazi ambalo kwa ujumla wake linaweza
kumpendeza kila mtu na kila rika.Kuanzia wanaume hadi wanawake, wazee
hadi watoto, ni vazi ambalo kwa hakika linamtoa kila mmoja wao.
Iwe harusini au msibani, iwe kwenye
hafla za kiserikali au shughuli za kawaida za kijamii, hakika vazi hili
ni la kipekee na ambalo haliwezi kumuangusha mvaaji.
Hebu cheki baadhi ya mishono ya vazi hili adhimu na si mbaya nawe ukajaribu siku moja kutokelezea katika vazi hili
No comments:
Post a Comment