Wanakijiji wa kijiji cha Nyamira wameamka na kukuta mwili wa mwanamke ukiwa umekatwa kichwa na kutelekezwa pamoja na kufungwa mikono kwa kamba...
Mwili huo ambao unaonyesha kuwa ni wa mwanamke mwenye miaka kati ya 25 hadi 35 amekutwa umevaa jeans pamoja na blouse nyeusi na kutupwa pembeni ya kijito cha maji mida ya saa 12 na nusu asubuhi.
Wanakijiji hao wamedai kushtushwa na tukio hilo na kusema kwamba ni kitu cha ajabu kwenye kijiji chao na polisi wa Kenya wametangaza familia yoyote itakayoona kuna mtu amepotea nyumbani kwao atoe taarifa mapema.
No comments:
Post a Comment