RAY AONA NOMA KUMBUSU LULU KISA MTOTO
STAA
wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema alipata wakati mgumu
kumpanga mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye filamu yake ambayo
walipaswa kucheza kama wapenzi kwa kuhofia kumbusu.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza
katika kituo kimoja cha runinga cha jijini Dar hivi karibuni, Ray
alisema licha ya kuwa Lulu alikuwa anastahili kuigiza katika sinema ya
Woman Principle miaka kadhaa iliyopita, aliona Lulu anafaa kutokana na
umakini wake lakini akaona bora amchukue Miss Tanzania namba 3, 2003,
Nargis Mohammed kwa kuhofia kupata aibu ya kuoneshana malavidavi na
Lulu.
Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Lulu
alikuwa na uwezo wa kumudu kipengele hicho, kipindi hicho alikuwa mdogo
sana, niliona ni jambo la aibu kidogo kumbusu mdomoni mtoto mdogo kama
yeye halafu ni kitu ambacho jamii itakaa ikitazame nikaona bora
nimchukue Nagris, Lulu nikampa sini nyingine,” alisema Ray.
Aliongeza
kuwa, kikubwa kilichomfanya avutiwe kucheza na Nagris ni kwa sababu ni
mwanamke ambaye katulia na hana skendo hivyo itamuongezea heshima na
mvuto wa kazi yake katika jamii.
No comments:
Post a Comment