MAMA KANUMBA AFUNGUKA NA KUSEMA KUWA"HAKUNA MSANII YEYOTE HAPA BONGO WA KUMFANANISHA NA MWANAYE KANUMBA"
MAMA
wa msanii aliyekuwa nguli wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba,
Flora Mtegoa amenyanyua kinywa chake na kutema cheche kuwa katika
mastaa wote wa filamu Bongo, hajaona hata mmoja wa kumfananisha na
mwanaye kimuonekano na hata katika uigizaji wake.
Flora Mtegoa.
Akipiga
stori na Mnyetishaji wetu mama Kanumba alisema hayo kutokana na mastaa
wengi kutamani awape nafasi ya kucheza kaAma Kanumba katika filamu yake
anayoiandaa inayohusu maisha ya mwanaye tangu utotoni, na kudai katika
wote hajaona mwenye kigezo cha kumpa nafasi hiyo.
Marehemu Steven Kanumba.
“Siyo
kwamba hawana kiwango kizuri cha kumfikia mwanangu, isipokuwa kwa
mtazamo wangu naona nikimshirikisha staa yoyote katika kipengele hicho
nitakuwa nimevurunda kazi yangu…nitaandaa tamasha maalumu la kumsaka
kijana anayefanana na Kanumba,” alisema mama huyo.
No comments:
Post a Comment