MSANII nyota wa filamu Bongo Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kuvunja urafiki na meneja wake Martin Kadinda kwa sababu kama kuna kitu chochote cha mafanikio nyuma yake yupo Kadinda.
Wema Sepetu ameuambia mtandao wa FilamCentral kuwa hana rafiki anayejua siri zake zaidi ya meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vema.
“Kadinda
ndo kila kitu kwangu, hata akiondoka na kukaa mbali na mimi kwa muda
mrefu ninapokutana naye tu, nitamweleza kila kitu toka siku ya mwisho
tuliyoachana, hivyo inakuwa kama sijapoteana naye,yaani ni kama vile
nipo naye kila siku iendayo kwa Mungu,”anasema Wema.
Msanii
huyu ameendelea kusema kwamba hata kampuni yake ya Endless Fame film
aliifungua kwa msaada wa Kadinda baada ya kumshauri kuwa kwa hadhi yake
anastahili kuwa na kampuni na aache kuigiza filamu za watu wengine.
No comments:
Post a Comment